Simba kurejea Jtano ijayo
Klabu ya Simba SC ya Tanzania inatarajia kurejea Dar es Salaam Jumatano ya Julai 31 kwaajili ya Simba Day 2024 na kuuanza rasmi msimu wa 2024 - 25.
Maadhimisho ya Simba Day yatafanyika Agosti 3 ambspo Wekundu hao wa Msimbazi watashuka dimbani kucheza na APR ya Rwanda.
Simba pia itatumia nafasi hiyo kutambulisha wachezaji wake wapya na wa zamani pamoja na Benchi lake la ufundi, mbali ya timu ys wanaume kucheza na APR, timu ya wanawake nayo itacheza mchezo wa kirafiki