Agosti 3 Simba kumtambulisha Mpanzu
Na Salum Fikiri Jr
Klabu ya Simba SC maarufu Wekundu wa Msimbazi Agosti 3 mwaka huu wakati wa tamasha lake la Simba Day inatarajia kumtambulisha winga Elie Mpanzu toka DR Congo kama mchezaji wake mpya.
Simba itamkata Willy Onana baada ya kocha wa Wekundu hao kumkataaa mazima na hivyo mabosi wa timu hiyo wamelazimika kumfuatilia Mpanzu na kuongeza dau analolitaka.
Simba ilishaachana na Mpanzu na kuamua kumtumia tiketi ya ndege Onana na kusafiri kuwafuata wenzake waliotangulia Misri, lakini jana Simbaisha kocha wa timu hiyo amemkataa waziwazi Onana na kutaka aletwe fasta mbadala wake ama sivyo timu itayumba kwenye Ligi na michuano ya kimataifa.
Jumamosi hii, kama mambo yakienda sawa atatambulishwa kwenye Simba Day, kama wakimpata Mpanzu watakwenda kugombea msimu ujao; Wakongomani wameniambia Mpanzu ni namba 10 ambaye muda mwingine anacheza kama winga kilisema chanzo changu