Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2014

KIVUMBI LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA

Picha
Katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya leo kuna kivumbi kingine ambapo CSKA Moscow itakuwa na kibarua kigumu pale watakapowakaribisha Bayern Munich. Wakati huo huo Man City waliopigwa bao moja na Bayern Munich watakutana na AC Roma iliyowapiga CSKA Moscow mabao matano katika mechi iliyopita. Paris St G ya Ufaransa wao wanakutana uso kwa uso na Barcelona Ukumbumbuke katika mechi ya wikendi iliyopita Paris St G walitoka sare na Ajax bao moja kwa moja. Ajax inakutana leo na Apoel Nic ambayo ilipigwa na Barcelona bao moja katika mechi ya awali.

KRISH FLAVOUR, MATONYA WAJA NA SHALABILEMA.

Picha
Msanii anayeibukia Omary Abdallah "Krish Flavour" ameibuka na ngoma matata 'Shalabilema' aliyomshirikisha mkali mwingine Seif Shaaban "Matonya" ambaye alipata kung'ara na nyimbo kadhaa. Akizungumza na gazeti hili Flavour amesema ameamua kuimba wimbo huo na kumshirikisha Matonya ambaye naye ameonyesha uwezo wake, Flavor ametaja maana ya Shalabilema ni mwanamke msafi anayejipenda ikiwa na maana sawa na neno Sharobalo. Flavour ameongeza kuwa muziki alianza tangia mwaka 2008 na aliachia wimbo wake wa kwanza uitwao 'namba moja' aliyomshirikisha Tanzanite na aliifanya katika studio ya Fire Music chini ya prodyuza more fire. Mwaka 2000 wimbo huo wa 'Namba moja' ndio ulianza kupigwa katika vituo kadhaa vya redio, ameongeza kuwa hadi sasa amesharekodi nyimbo zaidi ya 14 lakini bado hajapata bahati ya kukubalika na kupata mafanikio kama ilivyo kwa wasanii wengine waliofanikiwa. Ameongeza kuwa wimbo wake wa Shalabilema ambao amemshirikisha Matonya...

SIMBA YAANZA KUJIIMARISHA, YATANGAZA SEKRETALIETI YAKE

Picha
KLABU ya Simba SC imetangaza Sekretarieti yake mpya ambayo itakuwa na majukumu ya kiutawala na kuratibu shughuli zote za uendeshaji wa klabu. Taarifa iliyotolewa na Rais wa Simba SC, Evans Aveva imesems kwamba Sekretarieti hiyo itakuwa ikifanya kazi zake chini ya kamati ya utendaji ambayo imeundwa na Rais wa klabu, makamu wake na wajumbe wengine wa kuteuliwa na kuchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu wa klabu ya simba. Ameutaja muundo wa sekretarieti hiyo kuwa ni Katibu Mkuu Stephen Ally, Mhasibu Amos Juma Gahumeni, Ofisa Habari Humphrey Nyasio, Ofisa Operesheni, Stanley Philipo, Ofisa Utawala Hussein Mozzy, pamoja na Mtunza ofisi, Juma Issa Matari.

BATAROKOTA ACHAGULIWA BALOZI WA UTALII.

Picha
Na Mariam Libibo Aliyekuwa mshiriki wa KTMA Batarokota ambaye ni mwimbaji wa muziki wa asili amepata dili ya aina yake baada ya kuchaguliwa kuwa balozi katika taasisi ya Tanzania Tourism Promotion and Research Organazation. Akizungumza mara baada ya kuanza kazi, Batarokota amesema anafuraha kupata heshima hiyo kubwa hivyo ataitendea haki nafasi hiyo. Aidha batarokota amesema anatarajia kutambulisha singo nyingine mpya yenye miondoko ya asili.

MART NOOIJ ATANGAZA KIKOSI CHA KUIVAA BENIN

Picha
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij ameteua wachezaji 26 kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Kocha Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), safu ya ulinzi itaendelea kutegemea mabeki wa Yanga SC kwa mujibu wa kikosi alichoteua ambacho kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).

RODGERS AFURAHISHWA NA SARE

Picha
Mwalimu Brendan Rodgers amesema Liverpool wanarejelea ubora wao baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya maadui wa jadi Everton katika uga wao wa Anfield Jumamosi. Nahodha wao, Steven Gerrard, alifunga goli lake la 10 katika mechi 32 dhidi ya waasimu hao muda mfupi baada ya kugonga saa lakini kapteni mwenzake, Phil Jagielka, alifungulia kombora kali kunusuru timu yake katika muda wa majeraha. Liverpool waliomaliza nafasi ya pili musimu uliopita wameshinda mechi mbili pekee muhula huu baada ya mechi sita na Rodgers alitangaza walistahili ushindi.

MESSI AANDIKISHA REKODI NYINGINE BARCELONA

Picha
Nyota maarufu wa Argentina, Lionel Messi, alifunga bao lake la 400 katika mchezo wa kulipwa huku mwenzake wa Brazil, Neymar, akitia kizimbani matatu kwenye ngoma ambayo magwiji wa Uhispania, Barcelona, waliadhibu vikali Granada 6-0 Jumamosi. Mabingwa Atletico Madrid walipanda hadi nafasi ya pili, alama mbili nyuma ya Barca baada ya kupatia Sevilla kichapo chao cha kwanza kwa kuwafunga magoli manne bila jibu. Naye mchezaji bora zaidi duniani, Cristiano Ronaldo, aliendelea kuwa hatari mbele ya lango baada ya kufungia Real Madrid kwenye ushindi wao wa 2-0 ugenini Villareal kubakia alama nne nyuma ya viongozi na maadui wao wakuu. Barca waliendeleza mwanzo wao bila kufungwa huku wakionesha makali yao katika mashambulizi yalioongozwa na Messi na Neymar.

YANGA YAANZA KAZI,COUTINHO HABARI NYINGINE

Picha
Yanga ilipata ushindi wake wa kwanza wa ligi msimu huu baada ya kuifunga timu iliyobakiwa na wachezaji 10 uwanjani ya Tanzania Prisons kwa magoli 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Kiungo Mbrazil Andrey Coutinho aliiandikia Yanga goli la kwanza katika dakika ya 34 kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililompita ubavuni kipa Mohamed Omary. Mbrazil huyo aliyekosa mechi ya ufunguzi waliyopigwa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita, aliachia kombora hilo la umbali wa takriban mita 25 wakati akipiga 'fri-kiki' iliyokwenda moja kwa moja wavuni. Dakika tano baada ya goli hilo, Prisons walilazimika kucheza pungufu baada ya Jacob Mwakalabo kutolewa kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumkwatua winga Mrisho Ngasa nje kidogo mwa boksi la maafande hao. Mchezaji huyo pia alionywa pia kwa kadi ya njano dakika ya 24 baada ya kumkwatua kiungo Haruna Niyonzima katikati ya uwanja.

TP MAZEMBE AIBU TUPU, YATOLEWA NYUMBANI

Picha
Samatta ashindwa kufikia rekodi ya Mputu Timu Entente Setif ya Algeria sasa itapambana na AS Vita Club ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika fainali ya Klabu Bigwa barani Afrika baada ya kuiondoa TP Mazembe pia ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa faida ya magoli ya ugenini japo TP Mazembe ilishinda hapo jana mechi ya nusu fainali kwa magoli 3 - 2. Entete Setif na TP Mazembe zote zilimaliza nusu fainali kila moja ikiwa na magoli manne kwa manne,magoli mawili Setif iliyoyafunga ugenini imewasaidia kuwa timu iliyofunga magoli mengi ikiwa ugenini.

MAKALA: VIONGOZI WA SIMBA TAMBUENI MAJUKUMU YENU

Picha
Na Prince Hoza MWENENDO wa klabu ya Simba katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara si mzuri na umeanza kuwashitua wanachama na mashabiki wake, Simba imeanza ligi kuu vibaya kwa kutoka sare mfululizo katika mechi zake mbili ilizocheza katika uwanja wake wa nyumbani. Kocha wa Simba Mzambia Patrick Phiri: anapaswa kuachiwa majukumu yake mwenyewe na si kuingiliwa na viongozi kama ilivyo sasa

MASIKINI SIMBA! KIONGERA KUIKOSA YANGA OKTOBA 12

Picha
MSHAMBULIAJI Mkenya, Paul Raphael Kiongera anaweza kuukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wapinzani wa jadi, Yanga SC Oktoba 12, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hiyo inafuatia kuumia katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Jumapili Uwanja wa Taifa, Simba SC ikilazimishwa sare ya 2-2 na Coastal Union, licha ya kuongoza kwa 2-0 hadi mapumziko. Kiongera alitokea benchi dakika ya 67, lakini dakika mbili kabla ya filimbi ya mwisho akampisha Amri Kiemba baada ya kuumia, kufuatia kugongana na kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado.

OKWI AWAAMBIA YANGA WATAFUNGA MDOMO TU.

Picha
Licha ya kupika mabao yote ya Simba katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu waliyotoka 2-2 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi, mshambuliaji Emmanuel Okwi amesema hakuwa katika kiwango chake. Okwi, aliyejiunga na Simba dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili msimu huu akitoka Yanga, alisababisha mabao yote ya Simba juzi licha ya mashabiki wa Yanga kumzomea mwanzo mwisho jambo analoamini muda si mrefu watatulia baada ya kurejea katika makali yake.

CAF YAIFUNGIA JS KABYLIE MIAKA MIWILI

Picha
Klabu ya Algeria JS Kabylie imepigwa marufuku kushiriki mashindano yeyote kwa miaka miwili.Shirikisho la soka la barani Afrika CAF limefikia kauli hiyo baada ya kuuawa kwa mshambulizi wa Cameroon Albert Ebosse uwanjani mwezi uliopita. Ebosse alikufa baada ya kupurwa na jiwe baada ya mechi ya ligi kuu ya Algeria.

RODGERS AMTULIZA GERRARD LIVERPOOL

Picha
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza kuwa hana mashaka na Steven Gerrard baada ya kupoteza michezo mitatu kati ya mitano. Kapteni wa timu hiyo alihaha huku na kule kubadilisha upepo wa mchezo baada ya kutandikwa mabao matatu kwa moja siku ya jumamosi katika michuano ya ligi kuu ya England.

MAKALA: SIMBA IMEBUGI KWA DONALD MOSOTI

Picha
Na Prince Hoza LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) ilianza rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo karibu timu zote zilishuka dimbani siku ya jumamosi na jumapili, ufunguzi huo wa ligi ulianza jumamosi na siku ya jumapili kulichezwa mechi moja tu. Mabingwa wa zamani wa Tanzania bara Simba SC walishuka dimbani kukabiliana na mabingwa wa bara mwaka 1989 Coastal Union ya Tanga kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu zote mbili zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana mabao 2-2, Simba ikiutumia uwanja wake wa nyumbani ilianza vema kipindi cha kwanza kwa kufanikiwa kujipatia mabao yake mawili. Mabao ya Simba yaliwekwa kimiani na Shaaban Kisiga 'Marone' na Amissi Tambwe, magoli yote mawili yalitokana na juhudi binafsi za kiungo mshambuliaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi ambaye aliweza kupiga krosi iliyomkuta Tambwe na kuweka mpira kimiani.

WEMA SEPETU ATOSWA JUMLA NA DIAMOND, SASA MENINAH KUOLEWA

Picha
Habari mpya zinasema kuwa vikao vya harusi ya Diamond na Meninah ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva vimeanza kimya kimya nyumbani kwa mama Diamond huku mmoja wa wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond mwenyewe na Queen Darlin ambaye ni dada wa Diamond. Kwa mujibu wa Baabkubwa magazine  paparazzi wake alienda nyumbani kwa Diamond hivi juzi kati kufanya nae mahojiano hata hivyo hakumkuta Diamond lakini alimkuta mmoja wa watu wake wa karibu ambaye yupo pia upande wa Wema Sepetu. Chanzo hicho kilimwaga news kuwa hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema bali ndoa inayopangwa kwasasa ni ya Diamond na Meninah na vikao vimeanza kwa mama Diamond. Chanzo hicho kilisema kuwa Diamond na Meninah walikutana takribani miezi mitano iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo za Kili Awards 2014 ambapo wote walitumbuiza.

COASTAL UNION YAISHIKA SHARUBU SIMBA UWANJA WA TAIFA

Picha
Simba ilipoteza uongozi wake wa magoli mawili na kujikuta ikilazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya 'ndugu zao' wa Coastal Union ya Tanga katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Ikionekana kudhamiria kuwa na matokeo tofauti na ya mahasimu wao Yanga ambao juzi walikumbana na kipigo cha 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro, Simba walihitaji dakika sita tu za kwanza kupata bao la kwanza. Mchezaji mpya Shabani Kisiga aliifungia Simba goli la kuongoza kwa 'fri-kiki' tamu iliyokwenda moja kwa moja wavuni. Refa Jacob Adongo aliamuru adhabu hiyo baada ya Emmanuel Okwi kukwatuliwa na Selemani Rajab nje kidogo ya boksi la Coastal.

YANGA WAPEWA MTIHANI NA BODI YA LIGI, IKIFAULU KULAMBA MAMILIONI

Picha
YANGA SC wamepewa sharti moja tu na Bodi ya Ligi, ambalo wakitekeleza watapatiwa Sh. Milioni 155. Sharti gani hilo? Msimu uliopita Yanga SC walisusia fedha za haki ya matangazo ya Televisheni ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinazotolewa na Azam Media Limited kwa sababu wao walikuwa wanapinga kampuni hiyo kupewa Mkataba huo. Lakini jitihada zao za kuipinga Azam Media kurusha Ligi Kuu zilishindikana kutokana na ukweli kwamba walitoa ofa nzuri ambayo hakukuwa na kampuni iliyofikia hata nusu yake.

PELLEGRIN AMSHAMBULIA MOURINHO

Picha
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ameikejeli Chelsea kwa kucheza kama timu ndogo timu hizo zilipoambulia sare ya Moja kwa moja uwanjani Etihad. Andre Schurrle ndiye aliyeiweka Chelsea mbele kabla ya mchezaji wa akiba Frank Lampard kuisawazishia man City ambayo ilikuwa na wachezaji . Pellegrini, 61,alisema "nafikiri tulicheza dhidi ya timu ndogo iliyokuwa inalinda ngome yake wala haitaki kucheza mbele. Sio jambo la kufurahisha kamwe .

BALOTELLI MATATANI TENA UINGEREZA

Picha
Polisi nchini Uingereza wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio ambalo mshambulizi wa Liverpool kutoka Italia Mario Balotelli alitukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter. Polisi katika mji wa Merseyside wameanzisha uchunguzi kufuatia matusi hayo yaliyotokea baada ya mshambulizi huyo wa Liverpool kutuma ujumbe akiicheka kichapo cha Manchester United mikononi mwa timu ndogo ya Leicester siku ya jumapili.

YANGA HAWATOKI JUMAMOSI- MTIBWA SUGAR

Picha
Uongozi wa Mtibwa Sugar umesema hautishwi na kipigo cha 3-0 ambacho Yanga imekitoa kwa Azam FC 3-0 kabla ya mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu itakayozikutanisha kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumamosi. Ikitoka kushiriki michuano ya Kombe la Kagame, Azam FC ilikubali kichapo hicho dhidi ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na kocha wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili.

WENGER AKIRI DORTMUND WALISTAHILI USHINDI

Picha
Arsene Wenger Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameungama kuwa timu yake ilitepetea na walistahili kichapo cha 2-0 walichopokea Ujerumani mikononi mwa Borussia Dortmund kwenye mechi ya ufunguzi ya ligi ya mabingwa Jumanne. Ciro Immobile na Pierre-Emerick Aubameyang walipatia miamba hao wa Ujerumani alama zote tatu kwenye Kundi D kwenye uga wa Westfalenstadion baada ya wenyeji kulemea Arsenal kotoka kipenga cha kwanza. Ingawa walikosa makali yao ya kawaida, wana Gunners walipoteza nafasi nadra walizozipata na mwishowe, mwalimu wao alikiri waliwezwa na timu bora zaidi.

PHIRI AMKUBALI JAJA, AWATAKA SIMBA KUJIPANGA

Picha
Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema nyota wa Yanga, Genilson Santos ‘Jaja’ ni mshambuliaji hatari na mwenye akili nyingi anapofika golini. Phiri alimshuhudia Jaja akifunga mabao mawili na kuiongoza Yanga kushinda 3-0 dhidi ya Azam katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Mzambia huyo, Phiri, alilimbia gazeti hili kuwa licha ya watu wengi kumbeza Jaja, lakini ni mshambuliaji hatari anapolikaribia lango na hapaswi kukabwa na mabeki legelege kwani wakati wowote anaweza kufunga.

LIVERPOOL YAUA, ARSENAL MAJANGA

Picha
Mashindano ya kutafuta klabu bingwa ya bara la ulaya katika mchezo wa soka ilianza jana huku timu kadhaa zikishuka katika viwanja mbalimbali ili kuanza kuzitafuta point tatu muhimu Mabingwa watetezi Real Madrid iliialika FC Basel katika uwanja wa Benabeu na kuanza vyema mbio za kutetea taji hilo kwa kuwafunga wapinzani wao kwa jumla ya mabao 5-1 huku washambuliaji wake wote wakiweza kuzifumania nyavu za wapinzani wao. Katika viwanja vingine Liverpool imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad na kushuhudia mwanzo mzuri wa mshambuliaji Baloteli aliyefunga moja ya mabao hayo mawili.

WACHEZAJI MAN UNITED 'WAKESHA' KUANGALIA LIGI YA MABINGWA

Picha
KLABU ya Manchester United haimo kabia katika michuano ya Ulaya msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya saba katika Ligi Kuu ya England msimu uliopita.Pamoja na hayo, wachezaji wake wameendelea kuonyesha mapenzi na michano hiyo baada ya kukubakli kuchelewa kulala, ili waangalie mechi za Ligi ya Mabingwa. Kipa David de Gea na baadhi ya wachezaji wenzake jana walipoteza muda kwa ajili ya mechi za Ulaya. Kipa huyo wa kimataifa wa Hispania, ameposti picha akiwa na wachezaji wenzake Marcos Rojo, Rafael, Antonio Valencia, Andreas Pereira, Anderson, Angel di Maria, Ander Herrera na Juan Mata wakipata chakula huku wanaangalia mechi za Ligi ya Mabingwa.

PHIRI AMPONDA LOGARUSIC, LAKINI WABANWA MBAVU NA NDANDA

Picha
Kocha mkuu wa Simba ambaye yupo katika mwezi wa kwanza wa mkataba wa mwaka mmoja, Patrick Phiri amesema aliikuta timu hiyo ikiwa na mapungufu mengi. Phiri alichukua majukumu ya kuifundisha Simba baada ya uongozi wa rais Evans Aveva kumtimua Zdravko Logarusic 'Loga' kutokana na kukosa mafanikio ndani ya timu hiyo. Mbali na kutofanya vizuri, kocha huyo pia alikuwa akilalamikiwa na wachezaji na baadhi ya viongozi kwa kutukana wachezaji na kuwafokea kupita kiasi. Akizungumza mwishoni mwa wiki, Phiri alisema kikosi cha timu hiyo kilikuwa na mapungufu mengi, ikiwamo kukosa uimara katika ulinzi na kiungo.

MCHEZAJI WA YANGA AMGOMEA MANJI

Picha
Mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Yusuph ‘Tigana’, amesema Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji (pichani) ‘anaivuruga’ klabu hiyo. Tigana aliliambia gazeti hili juzi katika mahojiano maalumu kuwa Manji amekuwa akifanya uamuzi aliouita wa kibabe, ambao umekuwa ukichangia kuivuruga timu hiyo. Winga huyo wa zamani wa Yanga na timu ya taifa (Taifa Stars), alisema Yanga imekuwa ‘ikipelekwapelekwa’ na kiongozi huyo na kusisitiza kuwa amekuwa akifanya anavyotaka kwenye klabu hiyo huku Wanayanga wakikaa kimya kwa sababu ana fedha. “Yanga sasa inapotea sababu ya kiongozi mmoja tu, sababu ana fedha, ndani ya klabu kumekuwa na uamuzi ambao si wa wote unafanywa na mtu mmoja kisa ana fedha, hivyo anaamua kufanya anavyojisikia,” alisema Tigana na kuongeza.

AZAM FC YAAPA KUILIZA YANGA BILA MUUAJI WAKE JOHN BOCCO

Picha
Kocha msaidizi wa Azam Fc, Kally Ongara, amesema kuwa kikosi chake kitaifunga Yanga leo kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani licha ya kumkosa mshambuliaji nyota John Bocco 'Adebayor'. Bocco atakosa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi, lakini mchezaji wa zamani wa Yanga Ongara alisema hata bila kuwapo kwa nahodha na mshambuliaji wake huyo, Azam ina uwezo wa kuifunga Yanga kwenye Uwanja wa Taifa. "Kikosi changu kipo kamili (na) tunawafahamu Yanga. (Ingawa) Bocco hatakuwapo uwanjani lakini hiyo si sababu ya sisi kutuzuia kuifunga Yanga," alisema Ongara.

BALOTELLI AANZA KAZI LIVERPOOL IKIPIGWA KIDUDE NYUMBANI NA VILLA

Picha
BAO pekee la Gabby Agbonlahor dakika ya tisa siku tatu tangu asaini Mkataba mpya wa miaka minne, limeipa Aston Villa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Liverpool Uwanja wa Anfield jioni ya leo. Hicho kinakuwa kipigo cha pili msimu huu kwa Liverpool, baada ya awali kufungwa mabao 3-1 na Manchester City Uwanja wa Etihad. Mshambuliaji mpya, Mario Balotelli aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan, alichezea kwa mara ya kwanza Liverpool lakini hakuweza kuiepusha na kipigo hicho.

Shearer asema Welbeck atang'ara Arsenal

Picha
Mshambuliaji mpya wa kilabu ya Arsenal Danny Welbeck anaweza kufunga mabao 25 kwa msimu mmoja ,hayo ni matamshi ya aliyekuwa mshambuliaji wa England Allan Shearer. Wellbeck mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na kikosi cha The Gunners kutoka kilabu ya Manchester United kwa kitita cha pauni millioni 16 katika siku ya mwisho ya dirisha la kuwasajili wachezaji wa soka barani ulaya na anaweza kuanzishwa kwa mara ya kwanza dhidi ya watetezi wa ligi hiyo Manchester City siku ya jumamosi.

MARIN CILIC BINGWA US OPEN

Picha
Marin Cilic wa Croatia ameibuka bingwa wa US Open kwa kumfunga Kei Nishikori wa Japan Mpambano huo umechezwa katika uwanja wa Arthur Ashe Mjini New York Marekani. Cilic amepokea kombe la michuano ya tennis upande wa wanaume kwa mara ya kwanza baada ya kumshindilia mpinzani wake seti tatu za 6-3, 6-3 , 6-3. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya fainali za US Open ambapo mchezo wa mwisho unawakosa mmoja kati ya wachezaji wakali akiwemo Andy Murray, Novak Djokovic ama Roger Federer.

PHIRI AJIVUNIA KIONGERA, OKWI,ATAMBA KUZISURUBU YANGA, AZAM

Picha
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Simba, Mzambia Patrick Phiri amesema uwezo alioonyesha mshambuliaji Raphael Kiongera (pichani), kwa kushirikiana na Emmanuel Okwi umekifanya kikosi chake kuwa imara katika safu ya ushambuliaji. Kiongera na Okwi Jumamosi walionyesha ushirikiano mzuri kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya wakati Simba ikishinda 3-0. Akizungumza juzi, Phiri alisema Kiongera ameonyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo na kuelewana vema na Okwi tofauti na alipocheza sambamba na Elias Maguri katika kipindi cha kwanza.

HISPANIA YAIFUMUA MACEDONIA 5-1 KUFUZU EURO

Picha
HISPANIA imefufua makali, baada ya kuanza vyema kampeni za kufuzu Euro 2016 kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Macedonia. Kocha Vincente Del Bosque alianzisha wachezaji wanane waliokuwepo kwenye Euro 2012 na Sergio Ramos akafunga bao la kwanza kwa panalti dakika ya 16 baada ya David Silva kuangushwa kwenye eneo la hatari. Paco Alcacer akafunga la pili dakika ya 17 baada ya kazi nzuri ya Juanfran kumpiga chenga kipa. Juanfran akawapa wapinzani penalti iliyofungwa na Agim Ibraimi dakika ya 28 aliyemtungua vizuri Iker Casillas. Sergio Busquets akafunga bao la tatu dakika ya 45 na ushei, kabla ya Silva kufunga la nne dakika ya 50 na Pedro kufunga la tano dakika ya 90 na ushei. Silva sasa amefikisha mabao mengi zaidi kwa wachezaji ambao si washambuliaji kihistoria Hispania, mbali na Fernando Hierro.

DIAMOND AFANYA KUFURU NYINGINE, ASOMESHA WATOTO INTERNATIONAL SCHOOL

Picha
MSANII anayetamba kwa sasa katika ukanda wa Afrika mashariki Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Plutinum amefanya kufuru nyingine kufuatia kutangaza kuwapeleka shule wale watoto walioshinda katika shindano lake la kucheza Ngollo. Katika ukurasa wake wa Istragram amesema 'Kama unakumbukumbu nzuri wakati nafanya tamasha langu la Christmass na Ngololo niliuliza mtoto atakae cheza vizuri Ngololo na kushinda nimpe zawadi gani?. 'Na wengi walisema Nimuendeleze kielimu, Hawa ndio washindi wetu walioshinda siku ile, ambao siku ya leo niliwapeleka Rasmi katika Shule ya East Africa International School iliyopo Mikocheni Dar es salaam ili waanze Masomo yao, aliongeza.

YANGA WAMPELEKA OKWI FIFA, WAISHUTUMU TFF WADAI INAIBEBA SIMBA

Picha
UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema unapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji  kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru. Mwenyekiti wa Kamati  ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo. Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.

TAIFA STARS YAPIGWA 5-0 NA BURUNDI

Picha
Timu ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) iliendeleza unyonge kwa Burundi baada ya kulala 2-0 katika mechi yao ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwagasore mjini Bujumbura. Matokeo hayo yalimaanisha kwanza Stars sasa imefungwa jumla ya magoli 5-0 katika mechi mbili dhidi ya Burundi baada ya awali kupigwa 3-0 katika mechi ya kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, Aprili 26 mwaka huu. Kipigo hicho kutoka kwa Burundi inayoshika nafasi 129 katika viwango vya FIFA vya ubora wa soka duniani, kinatarajiwa kuishusha zaidi Tanzania, ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 110 duniani. Viwango vipya vya FIFA vitatoka Septemba 18.

EMMANUEL OKWI KIMEELEWEKA SIMBA, YADAIWA YANGA ILIVUNJA MKATABA WAKE TANGIA JANUARI MWAKA HUU

Picha
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana (Septemba 7 mwaka huu) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi. Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga, na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.

SERENA WILLAMS BINGWA US OPEN

Picha
Serena Williams Mcheza tennis Serena Williams wa Marekani ametwaa ubingwa wa US Open. Williams ameshinda katika mchezo uliofanyika usiku wa kuamkia leo baada ya kumtwanga Caroline Wozniacki wa Denmark kwa ushindi wa moja kwa moja.

ROONEY ATAKA WAANZE KWA NGUVU

Picha
Wayne Rooney  Wayne Rooney amekiri kwamba Uingereza hawawezi kuthubutu kuanza kwa upole kampeni yao ya kufuzu kwa Euro 2016 dhidi ya Uswizi Jumatatu. Timu hiyo ya Roy Hodgson itaelekea Basle ikihitaji sana kucheza vyema na kujipatia matokeo ya kufuta masikitiko yao Kombe la Dunia. Safari yao kwenda Euro Ufaransa itaanza kwa mechi ngumu dhidi ya Waswizi, ambao huenda wakawa wapinzani pekee wakali dhidi ya Uingereza Kundi E. Usiwzi – ambao walishindwa na Argentina kupitia goli la Angel di Maria dakika za mwisho za muda wa ziada katika mechi ya 16 bora Kombe la Dunia – wameorodheshwa wa tisa duniani na wanapigiwa upatu kushinda mechi hiyo ya Jumatatu uwanjani St Jakob-Park dhidi ya timu ya Uingereza ambao bado inaathiriwa na maruerue ya Kombe la Dunia.

PHIRI AIPELEKA SIMBA RWANDA

Picha
Wakati kocha wa Simba, Patrick Phiri, akisema kikosi cha timu yake sasa ni sawa na 'moto usioshikika', timu hiyo inasaka wapinzani kutoka Rwanda baada ya kufutika kwa mechi yao iliyopaswa kuchezwa keshokutwa Jumatano dhidi ya Big Bullets kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza jana, Phiri, alisema kuwa kikosi chake kimeiva na kiko tayari kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayo itaanza Septemba 20 mwaka huu. Phiri alisema kuwa kiwango kilichoonyeshwa na timu yake katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kilimfurahisha na kilikuwa cha juu.

SIMBA YAREJEA DAR KUIVAA GOR MAHIA

Picha
Timu ya Simba inarudi jijini Dar es Salaam kesho kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, huku kocha Patrick Phiri akitarajia kuwatumia washambuliaji wake wapya wa kigeni Mkenya Raphael Kiongera na Mganda Emanuel Okwi. Hata hivyo, Phiri atalazimika kumuanzisha mmoja kati yao ili acheze na Elias Maguli, ambaye atachukua nafasi ya Amissi Tambwe aliyekwenda kuichezea timu yake ya Taifa ya Burundi. Washambuliaji wote hao wamechelewa kujiunga na kambi hiyo kwani Okwi ameingia dakika za mwisho za usajili akitokea Yanga, wakati Kiongera akiwa kwao kuisaidia timu yake ya zamani, KCB katika baadhi ya mechi ili isishuke daraja.

TAIFA STARS WAPAA, TAYARI KULIPIZA KISASI KWA BURUNDI

Picha
Kikosi chenye wachezaji 20 cha timu ya taifa (Taifa Stars) kimeondoka nchini leo alfajiri kwenda Bujumbura, Burundi huku kocha wa timu hiyo, Mholanzi Mart Nooij akiahidi kulipa kisasi cha kufungwa 3-0 dhidi ya taifa hilo katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya 'Entamba Murugamba' itakayopigwa nchini humo Jumapili. Katika mechi iliyopita ya kirafiki iliyozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Aprili 26, mwaka huu, kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa "kimefinyangwafinyangwa" na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kulazimisha waanze wachezaji watano wa 'maboresho', kililala 3-0 dhidi ya Warundi na kuharibu pilau la sherehe zilizokuwa zimefana za Miaka 50 ya Muungano.

ALIYEMPIGA KICHWA MWAMUZI AENDA JELA

Picha
Ismail Gunduz Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kuto cheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani mwamuzi wa mchezo.

SIMBA YAKWAA KISIKI KWA OKWI TFF

Picha
Huku ikiwa tayari imewasilisha madai ya Dola 500,000 za Marekani, uongozi wa klabu ya Yanga jana uliwasilisha pingamizi rasmi dhidi ya mshambuliaji Emmanuel Okwi, ambaye Simba ilitangaza kumsajili. Katika malalamiko ya awali, Yanga pia imeomba Simba ifungiwe kwa kukiuka taratibu huku pia mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Uganda (Uganda Cranes) afungiwe kucheza soka. Habari ambazo zimepatikana jijini Dar es Salaam zinaeleza kuwa Yanga iliwasilisha pingamizi hilo katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikieleza kwamba Okwi bado ni mchezaji wake halali.

WAAMUZI ZANZIBAR KIMEELEWEKA

Picha
WAAMUZI 21 wanaochezesha soka visiwani Zanzibar wamefaulu katika mtihani wao wa utimamu wa mwili (Kopa Test) uliofanyika juzi visiwani Zanzibar. Mtihani huo ambao ulikuwa chini ya wakufunzi Muhsini Ali Kamara na Juma Ali David kutoka Zanzibar na mkufunzi kutoka Dar Es Salaam Riziki Majala, ulishirikisha waamuzi 25. Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa Soka Zanzibar (ZAFRA) Issa Ahmada Hija ‘Jogoo’ alisema kuwa waamuzi hao waliofaulu watachezesha ligi kuu ya Zanzibar pamoja na ligi daraja la kwanza na la pili Taifa. Aidha akizungumzia waamuzi wanne ambao wamefeli waamuzi waliofeli mtihani huo watapewa nafasi ya kutahiniwa tena mara baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu kumalizika.

LIVERPOOL YAINGAMIZA TOTTENHAM 3-0

Picha
Wachezaji Liverpool wakishangilia ushindi Ligi kuu ya England ambayo imendelea jumapili kwa timu sita kujitupa uwanjani katika michezo mitatu. Katika mechi ya kwanza Meneja wa Liverpool Brenden Rodgers alitimiza mechi yake 100 tangu aichukue usukani wa kuifundisha liverpool kwa kushuhudia timu yake ikiisambaratisha Tottenham Hotspur kwa jumla ya magoli 3 kwa 0.

ROJO NJIA PANDA KUKIPIGA MAN UNITED

Picha
Marcos Rojo anashindwa kuanza kuichezea Manchester United kwa madai ya tuhuma za mzozano uliozuka na jirani yake nchini Argentina mwaka 2010. Rojo, 24, alikamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 16 kutoka Sporting Lisbon siku 11 zilizopita, lakini uchunguzi wa makosa ya jinai unaoendelea dhidi yake unamaanisha hawezi kupewa viza (kibali) ya kufanyia kazi inayotakiwa Uingereza. Hata hivyo meneja wa Manchester United Louis van Gaal ana uhakika Rojo ataweza kucheza mechi dhidi ya QPR Septemba 14.

KAGAWA AREJEA DORTMUND

Picha
Kiungo kutoka Japan Shinji Kagawa amejiunga tena na Borussia Dortmund kutoka Manchester United kwa kiasi ambacho hakikutajwa. Mchezaji huyo, 25, amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo aliyoichezea kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 kabla ya kuhamia Old Trafford kwa pauni milioni 12. "Nafasi ilijitokeza ya kumsajili Shinji Kagawa kutoka Manchester United," amesema mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Michael Zorc.

OKWI KITU GANI BHANA, NGASSA ANATISHA KWA MABAO AFRIKA

Picha
WAKATI Ligi ya Mabingwa Afrika ikielekea hatua ya nusu fainali, straika Mrisho Ngassa wa Yanga bado anaongoza kwa ufungaji katika michuano hiyo akiwa na mabao sita. Ngassa amecheza mechi nne tu za ligi hiyo mbili dhidi ya Komorozine de Domoni ya Comoro na nyingine dhidi ya Zamalek ya Misri kisha timu yake ikatolewa. Ngassa alifunga mabao yote sita dhidi ya Komorozine ambapo alifunga matatu ‘hat trick’ jijini Dar es Salaam na mengine matatu katika marudiano mjini Mitsamiouli, Comoro. Katika orodha ya ufungaji iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Ngassa anafuatiwa na wachezaji wanne wenye mabao matano kila mmoja, lakini ni mmoja tu mwenye nafasi ya kumfikia. Wenye mabao matano na timu zao kwenye mabano ni Edward Sadomba wa Ahly Benghazi ya Libya, Haithem Jouini (Esperance, Tunisia), Iajour Mouhssine (Raja Club, Morocco) na Mubele Nodome wa AS Vita ya DR Congo.

BIN KLEB AANZA KUMFUNGIA KAZI OKWI

Picha
Baada ya Yanga 'kupigwa' na wapinzani wao wa jadi, Simba ambao wametangaza kumsajili kwa mara nyingine Mganda Emmanuel Okwi aliyeichezea msimu uliopita, hatimaye umeamua kumrejesha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Abdallah Bin Kleb, kuwa mjumbe wa kamati hiyo. Hata hivyo, mustakabali wa sakata la Okwi kukubaliwa kuichezea Simba au la linatarajiwa kutolewa ufafanuzi Septemba 6, mwaka huu wakati Kamati ya Mashindano na Haki za Wachezaji ya TFF itakapokutana. Wakati Bin Kleb akiwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ndiye aliyefanikisha usajili wa Okwi, huku akishinda vita ya kuwania pia saini ya Mbuyu Twite aliyekuwa amekula fedha za usajili za Simba kwa makubaliano ya kuichezea.