MAKALA: VIONGOZI WA SIMBA TAMBUENI MAJUKUMU YENU
Na Prince Hoza
MWENENDO wa klabu ya Simba katika msimamo wa ligi kuu
Tanzania bara si mzuri na umeanza kuwashitua wanachama na mashabiki wake, Simba
imeanza ligi kuu vibaya kwa kutoka sare mfululizo katika mechi zake mbili
ilizocheza katika uwanja wake wa nyumbani.
Kocha wa Simba Mzambia Patrick Phiri: anapaswa kuachiwa majukumu yake mwenyewe na si kuingiliwa na viongozi kama ilivyo sasa
Simba imeanza ligi kwa kucheza na Coastal Union Septemba 21
ambapo katika mchezo huo licha ya kuongoza katika kipindi cha kwanza kwa mabao
2 kwa 0 ilijikuta inazlazimishwa sare ya mabao 2-2 na kuambulia pointi moja.
Katika mchezo huo wa kwanza Simba ilishusha kikosi chake
chote cha kwanza chenye wachezaji tegemeo, chini ya kocha wake mkuu Mzambia
Patrick Phiri, Simba iliingia uwanjani ikishangiliwa na mashabiki wake ambao
walikua na shauku kubwa kuiona timu yao ikirejea kwenye makali yake tofauti na
msimu uliopita ambapo iliangukia nafasi ya nne.
Simba ya msimu uliopita ilianza ligi kwa kucheza na Rhino
Rangers ya Tabora na mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi
mjini Tabora, Simba ilitoka sare ya kufungana 2-2 na Rhino lakini ilikosa
huduma ya wachezaji wake wa kimataofa kutokana na vibali vyao vya kufanyia kazi
kutokamilika.
Wachezaji hao ni Amissi Tambwe aliyeajiliwa kwa mara ya
kwanza akitokea Vital’O ya Burundi na Gilbert Kaze, Ikiwa chini yake Mzalendo
Abdallah King Kibaden Simba ilielekea jijini Arudha kukwaruzana na JKT Oljoro
na kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Hata hivyo Simba katika mechi mbili za mwanzo wa ligi
ilijikusanyia pointi nne, uongozi wa aliyekuwa mwenyekiti wa Wekundu hao wa
Msimbazi Ismail Aden Rage ulimal.iza muda wake na kuacha majeraha makubwa,
Wanasimba wanakumbukumbu mbaya ya kutopata nafasi ya kushiriki michuano ya
kimataifa misimu miwili mfululizo.
Rais Aveva: hii ndio kazi yako kuwahutubia wanachama katika vikao mbalimbali na kuwapa taarifa za maendeleo kama vile ujenzi wa uwanja wa Bunju
Mbali na kutopata nafasi ya ushiriki wa kmichuano ya
kimataifa,Migogoro ilizidi kuiandama klabu hiyo kila kukicha, wachezaji wote
muhimu walikuwa wakiuzwa kwa klabu nyingine na kuiacha Simba ikisaliwa na
patupu, Simba haikuwa ile yenye makali yake kama ilivyokuwa katika miaka ya
nyuma ambapo Simba ilitingisha ndani na nje ya nchi.
Tatizo kubwa lililoitafuna Simba na kupelekea kupoteza
mwelekeo ni viongozi wake kutojitambua, kiongozi badala ya kufanya kazi yake
kama kiongozi anajikuta anaingilia majukumu ya mwalimu na kupelekea kupotea kwa
taaluma na timju kufanya vibaya.
Imekuwa jambo la kawaida kuona kiongozi wa kuchaguliwa na
wanachama anadiriki kumpangia kikosi mwalimu , pia ni jambo lililozoeleka
viongozi kuhusika moja kwa moja na mambo ya usajili wakati mwenye jukumu hilo
ni kocha na benchi lake zima la ufundi.
Uongozi wa Rage uliondoka na kupisha safu mpya ya uongozi
ambayo ilipewa matumaini makubwa kuibadili klabu hiyo, Evans Elieza Aveva
alichaguliwa kuhsika nafasi ya urais wakati makamu wake ni Geofrey Nyange
Kaburu, safu hiyo ilionekana kuwa makini na hasa historia iliyokuwa nayo tangia
miaka ya nyuma.
Kaburu anakubalika na Wanasimba wote kutokana na mchango
mkubwa alionao kwa klabu hiyo, Kaburu anasifika kwa kufanya usajilimzuri na
makini ulioiwezesha Simba kung’ara ndani na nje ya Tanzania, Kaburu aliwezesha kupatikana kwa kikosi imara
cha Simba kilichowezesha kutamba hapa nchini.
Ujio waokwa mara nyingine umeweza kuwapa faraja mashabiki wa
Simba ambao walikuwa wanyonge kwa muda mrefu, Soka la sasa limebadilika kwa kiasi kikubwa
tofauti na miaka ile ambapo Simba iliweza kutamba ndani na nje ya Tanzania.
Kwa sasa karibu vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu bara
vimejipanga kushiriki ligi hiyo kutokana na ufadhili mkubwa unaotolewa na
wadhamini kadhaa wa ligi hiyo, vilabu vidogo kama vinavyofahamika kwa sasa
vinawezeshwa mamimilioni ya fedha kutoka kwa wadhamini wakuu wa ligi hiyo
kampuni ya simu za mkononi Vodacom pamoja na Azam TV.
Pia wadhamini wengine kama Bin Slum Tyres nao wamewekeza
mamilioni yao kwa baadhi ya vilabu hivyo kuongeza ushindani, miaka ile ya nyuma
Simba SC pekee ndio iliyokuwa na wadhamnhi lukuki na kuweza kufanya vizuri
katika soka la nchi hii na nje ya mipaka.
Kazi ipo uwanjani tu na si kwingine, wachezaji wa klabu ya Simba wakifurahia moja ya majukumu yao uwanjani.
Simba ilikuwa na wadhamini kama Mohamed Interprises, Simba
Cement na benki ya NBC, wadhamini hao waliisaidia Simba kwa hali na mali hivyo
kuweza kusajili wachezaji nyota na kufanya vizuri, wapinzania wake wakuu Yanga
hawakuwa na mfadhili na walitegemea fedha za milangoni.
Timu nyingine zilizokuwa zikishiriki ligi kuu zilikuwa
ombaomba zaidi ya Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na timu za majeshi zilizokuwa na
nguvu za kujiendesha, lakini safari hii kila klabu inajiweza kiuchumi, ni ngumu
sana kutegemea mpira wa fitina kama unavyojulikana kwa miamba ya soka nchini
Simba na Yanga.
Katika zama hizi soka linategemea zaidi sayansi na
teknolojia, ni wakati wa wataalamu kufanya kazi zao na viongozi kuendesha
jahazi, nilifurahia sana ujio wa Aveva ambaye ni mfuasi wa kundi la marafiki wa
Simba maarufu F.O.S, kundi hilo limejizolea mashabiki wengi kutokana na hamasa
yake ndani ya Simba.
Aveva ni memba wa kundi hilo na ndiye rais wa Simba hivyo
nguvu nyingi zinatoka kwa kundi hilo, cha kushangaza ni kwamba tangia alipoingia
madarakani sijaona juhudi zozote za kimaendeleo, Aveva na wenzake wamesahau
majukumu yao badala ya kufanya kazi zinazowahusu wamejikita katika benchi la
ufundi.
Kazi za viongozi si kuisimamia
timu uwanjani, kazi ya kuisimamia timu inafanywa na kocha na benchi lake la
ufundi, masuala mazima ya usajili yote ni kocha, viongozi wanapaswa kujua timu
inaweka kambi wapi, uwanja unapatikana wapi, wafadhili tutawapataje nk, lakini
akina Kaburu na wenzake wote wanashinda wote na timu uku wakiingilia usajili wa
wachezaji na na ndicho kilichopelekea Donald Mosoti kuachwa wakati ndiye beki muhimu
kwa wakati huu ndani ya Simba, Ni hayo tu, tuonane wiki ijayo.