SIMBA YAANZA KUJIIMARISHA, YATANGAZA SEKRETALIETI YAKE

KLABU ya Simba SC imetangaza Sekretarieti yake mpya ambayo itakuwa na majukumu ya kiutawala na kuratibu shughuli zote za uendeshaji wa klabu.

Taarifa iliyotolewa na Rais wa Simba SC, Evans Aveva imesems kwamba Sekretarieti hiyo itakuwa ikifanya kazi zake chini ya kamati ya utendaji ambayo imeundwa na Rais wa klabu, makamu wake na wajumbe wengine wa kuteuliwa na kuchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu wa klabu ya simba.

Ameutaja muundo wa sekretarieti hiyo kuwa ni Katibu Mkuu Stephen Ally, Mhasibu Amos Juma Gahumeni, Ofisa Habari Humphrey Nyasio, Ofisa Operesheni, Stanley Philipo, Ofisa Utawala Hussein Mozzy, pamoja na Mtunza ofisi, Juma Issa Matari.


Aveva amesema kwamba Sekretarieti hiyo imeshaanza kazi kuanzia Septemba 1, hivyo Kamati ya Utendaji inawaomba wanachama, washabiki na wadau wote wa michezo kuipa sekretarieti hiyo ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake katika klabu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA