TAIFA STARS YAPIGWA 5-0 NA BURUNDI

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) iliendeleza unyonge kwa Burundi baada ya kulala 2-0 katika mechi yao ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwagasore mjini Bujumbura.

Matokeo hayo yalimaanisha kwanza Stars sasa imefungwa jumla ya magoli 5-0 katika mechi mbili dhidi ya Burundi baada ya awali kupigwa 3-0 katika mechi ya kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, Aprili 26 mwaka huu.

Kipigo hicho kutoka kwa Burundi inayoshika nafasi 129 katika viwango vya FIFA vya ubora wa soka duniani, kinatarajiwa kuishusha zaidi Tanzania, ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 110 duniani. Viwango vipya vya FIFA vitatoka Septemba 18.


Burundi ilipata bao la kwanza  katika sekunde ya 40 kupitia kwa Saidi Ntibazonkiza kabla ya Ndikumana Yusufu kufunga la pili kwa kichwa akimalizia mpira wa kona iliyopigwa na Ndikumasabo Styve katika dakika ya 24.

Vikosi katika mechi hiyo vilikuwa; Taifa Stars: Deogratius Munishi 'Dida', Shomary Kapombe, Haroub Nadir, Saidi Morad, Joram Mgeveke, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto, Mcha Khamis, Amri Kiemba Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.

Burundi: Mbonihankuy Innocent, Ntibanzonkiza Saidi, Kiza Fataki, Hakizimana Issa, Rachidi Leo, Ndikumana Yusufu, Kwizera Pierre, Ndikumasabo Styve, Hussein Shabani, Kavumbangu Didier na Nshimirimana David.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA