ROONEY ATAKA WAANZE KWA NGUVU

Wayne Rooney 

Wayne Rooney amekiri kwamba Uingereza hawawezi kuthubutu kuanza kwa upole kampeni yao ya kufuzu kwa Euro 2016 dhidi ya Uswizi Jumatatu.

Timu hiyo ya Roy Hodgson itaelekea Basle ikihitaji sana kucheza vyema na kujipatia matokeo ya kufuta masikitiko yao Kombe la Dunia.

Safari yao kwenda Euro Ufaransa itaanza kwa mechi ngumu dhidi ya Waswizi, ambao huenda wakawa wapinzani pekee wakali dhidi ya Uingereza Kundi E.
Usiwzi – ambao walishindwa na Argentina kupitia goli la Angel di Maria dakika za mwisho za muda wa ziada katika mechi ya 16 bora Kombe la Dunia –

wameorodheshwa wa tisa duniani na wanapigiwa upatu kushinda mechi hiyo ya Jumatatu uwanjani St Jakob-Park dhidi ya timu ya Uingereza ambao bado inaathiriwa na maruerue ya Kombe la Dunia.


Ushindi usio wa kuridhisha wa 1-0 mechi ya kupimana nguvu na Norway katikati ya wiki haukupokelewa vyema, na bosi wa Uingereza Hodgson alionekana asiye na furaha na kuwajibu kwa ukali wanahabari waliouliza maswali kutokana na ukosefu wa makombora ya kulenga goli.

Kutokana na hayo, nahodha wa Uingereza Rooney anajua wenzake hawawezi wakathubutu kuruhusu mabaya ya Kombe la Dunia yazidi kuendelea.

“Ni muhimu kuanza kampeni ya kufuzu kwa matokeo mazuri,” Rooney alisema.
“Ni muhimu kujaribu na kushinda mechi, lakini nafikiri kukosa kushindwa na kuwanyima Uswizi uongozi kutoka kwa mechi ya kwanza ni muhimu.”

Kutoridhishwa kwa wananchi Uingereza baada ya Kombe la Dunia kulijionyesha Jumatano ambapo mashabiki waliofika kutazama mechi ya kirafiki dhidi ya Norway uwanjani Wembley ndio wachache zaidi kufika tangu kufunguliwa kwa uwanja huo 2007.

Kuharibu mambo zaidi, mashabiki 40 181 waliofika hawakufurahishwa na uchezaji wa Uingereza ambao ulikuwa duni.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA