AZAM FC YAAPA KUILIZA YANGA BILA MUUAJI WAKE JOHN BOCCO
Kocha msaidizi wa Azam Fc, Kally Ongara, amesema kuwa kikosi chake kitaifunga Yanga leo kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani licha ya kumkosa mshambuliaji nyota John Bocco 'Adebayor'.
Bocco atakosa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi, lakini mchezaji wa zamani wa Yanga Ongara alisema hata bila kuwapo kwa nahodha na mshambuliaji wake huyo, Azam ina uwezo wa kuifunga Yanga kwenye Uwanja wa Taifa.
"Kikosi changu kipo kamili (na) tunawafahamu Yanga. (Ingawa) Bocco hatakuwapo uwanjani lakini hiyo si sababu ya sisi kutuzuia kuifunga Yanga," alisema Ongara.
Alisema wamekiandaa vizuri kikosi chao na wapo tayari kuwakabili Yanga kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Bara.
Kwa kukosekana kwa Adebayor ambaye pia ndiye mfungaji tegemeo, kikosi cha Azam kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog kitawategemea zaidi Kipre Tchetche, Leonel Saint Preux na Khamis Mcha kwenye ushambuliaji.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo alisema ingawa timu itakuwa bila Jerry Tegete na Mbrazili Coutinho, bado ana wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa.
Yanga wanaingia kwenye mchezo wa leo unaokutanisha timu mbili zilizoshika nafasi mbili za kwanza msimu uliopita wakiwa na kumbukumbu ya kuwafunga mabingwa wa Bara Azam 1-0 kwenye mechi kama hiyo mwaka jana.