WACHEZAJI MAN UNITED 'WAKESHA' KUANGALIA LIGI YA MABINGWA

KLABU ya Manchester United haimo kabia katika michuano ya Ulaya msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya saba katika Ligi Kuu ya England msimu uliopita.Pamoja na hayo, wachezaji wake wameendelea kuonyesha mapenzi na michano hiyo baada ya kukubakli kuchelewa kulala, ili waangalie mechi za Ligi ya Mabingwa. Kipa David de Gea na baadhi ya wachezaji wenzake jana walipoteza muda kwa ajili ya mechi za Ulaya.

Kipa huyo wa kimataifa wa Hispania, ameposti picha akiwa na wachezaji wenzake Marcos Rojo, Rafael, Antonio Valencia, Andreas Pereira, Anderson, Angel di Maria, Ander Herrera na Juan Mata wakipata chakula huku wanaangalia mechi za Ligi ya Mabingwa.


Mzuia michomo huyo wa zamani wa Atletico Madrid ameposti picha hiyo kwenye akaunti yake ya Twitter akiambatanisha na ujumbe: "Chakula cha usiku na timu"!.

Watazamaji; David de Gea akiwa na wachezaji wenzake Marcos Rojo, Rafael, Antonio Valencia, Andreas Pereira, Anderson, Angel di Maria, Ander Herrera na Juan Mata wakipata chakula cha usiku huku wakiangalia Ligi ya Mabingwa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA