OKWI KITU GANI BHANA, NGASSA ANATISHA KWA MABAO AFRIKA

WAKATI Ligi ya Mabingwa Afrika ikielekea hatua ya nusu fainali, straika Mrisho Ngassa wa Yanga bado anaongoza kwa ufungaji katika michuano hiyo akiwa na mabao sita.

Ngassa amecheza mechi nne tu za ligi hiyo mbili dhidi ya Komorozine de Domoni ya Comoro na nyingine dhidi ya Zamalek ya Misri kisha timu yake ikatolewa.

Ngassa alifunga mabao yote sita dhidi ya Komorozine ambapo alifunga matatu ‘hat trick’ jijini Dar es Salaam na mengine matatu katika marudiano mjini Mitsamiouli, Comoro.

Katika orodha ya ufungaji iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Ngassa anafuatiwa na wachezaji wanne wenye mabao matano kila mmoja, lakini ni mmoja tu mwenye nafasi ya kumfikia.

Wenye mabao matano na timu zao kwenye mabano ni Edward Sadomba wa Ahly Benghazi ya Libya, Haithem Jouini (Esperance, Tunisia), Iajour Mouhssine (Raja Club, Morocco) na Mubele Nodome wa AS Vita ya DR Congo.


Hata hivyo, Nodome ndiye mwenye nafasi kubwa ya kumfikia Ngassa kwani timu yake imefika nusu fainali na itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Sfaxien ya Tunisia Septemba 20, mwaka huu DR Congo.

Nusu Fainali nyingine itazikutanisha ES Setif ya Algeria na TP Mazembe ya DR Congo siku hiyo hiyo nchini Algeria.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA