TP MAZEMBE AIBU TUPU, YATOLEWA NYUMBANI



Samatta ashindwa kufikia rekodi ya Mputu

Timu Entente Setif ya Algeria sasa itapambana na AS Vita Club ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika fainali ya Klabu Bigwa barani Afrika baada ya kuiondoa TP Mazembe pia ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa faida ya magoli ya ugenini japo TP Mazembe ilishinda hapo jana mechi ya nusu fainali kwa magoli 3 - 2.

Entete Setif na TP Mazembe zote zilimaliza nusu fainali kila moja ikiwa na magoli manne kwa manne,magoli mawili Setif iliyoyafunga ugenini imewasaidia kuwa timu iliyofunga magoli mengi ikiwa ugenini.


Nayo AS Vita Club imetinga hatua hiyo fainali baada ya kuibamiza CS Sfaxien ya Tunisia siku ya jumamosi kwa ushindi wa jumla wa magoli 4 - 2.

Hata hivyo mashabiki TP Mazembe pamoja na timu yao kutolewa katika mashindano hayo ambayo sasa itachezea mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wamesema wataiunga mkono AS Vita Club ambayo ni timu nyingine kutoka DRC.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA