DIAMOND AFANYA KUFURU NYINGINE, ASOMESHA WATOTO INTERNATIONAL SCHOOL


MSANII anayetamba kwa sasa katika ukanda wa Afrika mashariki Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Plutinum amefanya kufuru nyingine kufuatia kutangaza kuwapeleka shule wale watoto walioshinda katika shindano lake la kucheza Ngollo.

Katika ukurasa wake wa Istragram amesema 'Kama unakumbukumbu nzuri wakati nafanya tamasha langu la Christmass na Ngololo niliuliza mtoto atakae cheza vizuri Ngololo na kushinda nimpe zawadi gani?.

'Na wengi walisema Nimuendeleze kielimu, Hawa ndio washindi wetu walioshinda siku ile, ambao siku ya leo niliwapeleka Rasmi katika Shule ya East Africa International School iliyopo Mikocheni Dar es salaam ili waanze Masomo yao, aliongeza.



'Niliona ni vyema kama mtoto yupo shule ya kawaida nimuhamishe international school ili niweze kumsaidia elimu bora zaidi...Niushkuru pia uongozi Mzima na wanafunzi wa Shule ya East Africa International School kwa kuwapokea vizuri.

Pichani kama unavyoona ni wale watoto walioshinda katika shindano la kucheza Ngololo wakiwa na wazazi wao, Diamond anawasomesha International School

Diamond sasa anajijengea heshima nyingine mbali na kutamba katika muziki, hatua aliyoichukua inapaswa kuigwa na wasanii wengine wenye mafanikio kama yake kwani kumsomesha shule mtoto wa mwenzio ni jambo la kujivunia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA