PELLEGRIN AMSHAMBULIA MOURINHO

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ameikejeli Chelsea kwa kucheza kama timu ndogo timu hizo zilipoambulia sare ya Moja kwa moja uwanjani Etihad.

Andre Schurrle ndiye aliyeiweka Chelsea mbele kabla ya mchezaji wa akiba Frank Lampard kuisawazishia man City ambayo ilikuwa na wachezaji . Pellegrini, 61,alisema "nafikiri tulicheza dhidi ya timu ndogo iliyokuwa inalinda ngome yake wala haitaki kucheza mbele.

Sio jambo la kufurahisha kamwe .


Wachezaji wangu 10 walilinda ngome yao na kupata bao la kusawazisha hadi tamati ya mechi.''

Pellegrini alifananisha mchezo wa Chelsea na ule wa Stoke ambayo iliilaza City 1-0 mwezi uliopita nyumbani kwao.

''Nafkiri tulicheza dhidi ya timu sawa na ile ya Stoke .Ilikuwa vigumu sana kwetu kufunga bao kwa sababu walikuwa wanalinga ngome yao badala ya kucheza mchezo wa hadhi inayostahili''

Sina haja ya kuwatathmini hata kidogo hilo nawachia timu zingine ''

City ilitoka nyuma na kusawazisha hata baada ya mlinzi wa kutegemewa Pablo Zabaleta kuoneshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea visivyo mshambulizi mpya wa Chelsea Diego Costa.

Kwa upande wake kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikataa kata kata kujibu madai hayo ya Pellegrini akisema ''mbona yeye husema kuwa hazungumzi kuhusi mimi na timu yangu ilihali anaendelea kupiga domo ?

Usiniulize chochote kumhusu Manuel"

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA