KAGAWA AREJEA DORTMUND

Kiungo kutoka Japan Shinji Kagawa amejiunga tena na Borussia Dortmund kutoka Manchester United kwa kiasi ambacho hakikutajwa.

Mchezaji huyo, 25, amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo aliyoichezea kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 kabla ya kuhamia Old Trafford kwa pauni milioni 12.

"Nafasi ilijitokeza ya kumsajili Shinji Kagawa kutoka Manchester United," amesema mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Michael Zorc.


"Bila shaka yoyote tuliamua kumsajili tena mchezaji huyu mwenye ubora." Ameongeza Zorc.

Kagawa alifunga magoli sita katika mechi 57 alizocheza Manchester United katika kipindi cha miaka miwili ambacho hakuweza kujikita katika kikosi cha kwanza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA