PHIRI AMPONDA LOGARUSIC, LAKINI WABANWA MBAVU NA NDANDA

Kocha mkuu wa Simba ambaye yupo katika mwezi wa kwanza wa mkataba wa mwaka mmoja, Patrick Phiri amesema aliikuta timu hiyo ikiwa na mapungufu mengi.

Phiri alichukua majukumu ya kuifundisha Simba baada ya uongozi wa rais Evans Aveva kumtimua Zdravko Logarusic 'Loga' kutokana na kukosa mafanikio ndani ya timu hiyo.

Mbali na kutofanya vizuri, kocha huyo pia alikuwa akilalamikiwa na wachezaji na baadhi ya viongozi kwa kutukana wachezaji na kuwafokea kupita kiasi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, Phiri alisema kikosi cha timu hiyo kilikuwa na mapungufu mengi, ikiwamo kukosa uimara katika ulinzi na kiungo.


"Wakati tupo Zanzibar nilifanyia kazi mapungufu niliyoyaona... timu haikuwa nzuri na hakukuwa na muunganiko mzuri," alisema.

"Lakini kwa sasa timu imekamilika kwa kiasi kikubwa na mpira unachezwa," alisema Phiri.

Alisema kuwa kila idara imekamilika kwenye kikosi chake isipokuwa mapungufu madogo madogo kwenye safu ya ushambuliaji.

"Tunatengeneza nafasi nyingi lakini umaliziaji umekuwa si mzuri, bado sijaridhishwa.
"Ni mambo madogo na nitaanza kuyafanyia kazi tukitoka Mtwara."

Simba ilikuwa Mtwara ambako jana ilicheza mechi ya kirafiki na Ndanda iliyopanda daraja la ligi kuu msimu huu kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Wakati huo huo Simba jana ilishindwa kutamba mbele ya timu iliyopanda daraja la Ndanda FC ya Mtwara baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona katika mchezo wa kirafiki wa kuadhimisha siku ya Ndanda Day

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA