CAF YAIFUNGIA JS KABYLIE MIAKA MIWILI

Klabu ya Algeria JS Kabylie imepigwa marufuku kushiriki mashindano yeyote kwa miaka miwili.Shirikisho la soka la barani Afrika CAF limefikia kauli hiyo baada ya kuuawa kwa mshambulizi wa Cameroon Albert Ebosse uwanjani mwezi uliopita.

Ebosse alikufa baada ya kupurwa na jiwe baada ya mechi ya ligi kuu ya Algeria.


Marufuku hiyo inatarajiwa kuathiri pakubwa Kabylie ambayo ilikuwa imefuzu kwa kombe la mabingwa barani Afrika mwakani baada ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka uliopita.Ebosse alikufa baada ya kugongwa na jiwe kichwani baada ya mechi ya ligi
Caf vilevile imeratibua kuanzisha tuzo kwa heshima yake Ebosse.

Klabu hiyo tayari imepigwa marufuku ya kucheza katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu wote wa 2014-2015 .

Aidha mashabiki wake hawawezi kushuhudia mechi yake yeyote nyumbani wala ugenini.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA