MESSI AANDIKISHA REKODI NYINGINE BARCELONA



Nyota maarufu wa Argentina, Lionel Messi, alifunga bao lake la 400 katika mchezo wa kulipwa huku mwenzake wa Brazil, Neymar, akitia kizimbani matatu kwenye ngoma ambayo magwiji wa Uhispania, Barcelona, waliadhibu vikali Granada 6-0 Jumamosi.
Mabingwa Atletico Madrid walipanda hadi nafasi ya pili, alama mbili nyuma ya Barca baada ya kupatia Sevilla kichapo chao cha kwanza kwa kuwafunga magoli manne bila jibu.

Naye mchezaji bora zaidi duniani, Cristiano Ronaldo, aliendelea kuwa hatari mbele ya lango baada ya kufungia Real Madrid kwenye ushindi wao wa 2-0 ugenini Villareal kubakia alama nne nyuma ya viongozi na maadui wao wakuu.

Barca waliendeleza mwanzo wao bila kufungwa huku wakionesha makali yao katika mashambulizi yalioongozwa na Messi na Neymar.


Neymar alifungua udhia dakika ya 26 baada ya kutimuka mbele na kuachilia mkwaju uliobadilishwa mwelekeo na kuishia kizimbani na beki Jean-Sylvain Babin.

Messi aliunganisha goli la saba musimu baada ya krosi yake kupata kichwa cha Ivan Rakitic aliyefunika mpira wavuni kabla ya Neymar kutia ndani la tatu kufikia kipindi cha kwanza.

Barca waliendelea na mshambulizi mazito na Neymar alipata lake la tatu baada ya kupokea mpira kutoka kisigino cha Messi kabla ya staa huyo wa Argentina kukamilisha adhabu alipopokonya ngome ya Granada mpira na kutimuka hadi kisanduku na kuzamisha ndani ya neti.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA