ROJO NJIA PANDA KUKIPIGA MAN UNITED
Marcos Rojo anashindwa kuanza kuichezea Manchester United kwa madai ya tuhuma za mzozano uliozuka na jirani yake nchini Argentina mwaka 2010.
Rojo, 24, alikamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 16 kutoka Sporting Lisbon siku 11 zilizopita, lakini uchunguzi wa makosa ya jinai unaoendelea dhidi yake unamaanisha hawezi kupewa viza (kibali) ya kufanyia kazi inayotakiwa Uingereza.
Hata hivyo meneja wa Manchester United Louis van Gaal ana uhakika Rojo ataweza kucheza mechi dhidi ya QPR Septemba 14.
Awali iliripotiwa kuwa utata kuhusu mmiliki wa tatu wa mchezaji huyo ndio sababu ya kucheleweshwa kwa kibali chake.
Hata hivyo Chama cha Soka cha England FA tayari kimetoa chetu chake cha uhamisho wa kimataifa na hakuna tatizo lolote la umiliki wa tatu.
Rojo aliingia Uingereza kukamilisha uhamisho wake kwa kutumia viza ya utalii.
Sheria za uhamiaji zinahitaji kila anayeingia Uingereza kufanya kazi kuwa na visa ya kufanyia kazi.
Rojo kwa sasa yuko mjini Madrid, Uhispania, akisubiri kufanya usaili na maafisa wa ubalozi wa Uingereza ili kupata kibali hicho.
Maafisa watapitia tuhuma za kuzozana na jirani yake huyo mwaka 2010 kabla ya kutoa viza hiyo.