BATAROKOTA ACHAGULIWA BALOZI WA UTALII.

Na Mariam Libibo

Aliyekuwa mshiriki wa KTMA Batarokota ambaye ni mwimbaji wa muziki wa asili amepata dili ya aina yake baada ya kuchaguliwa kuwa balozi katika taasisi ya Tanzania Tourism Promotion and Research Organazation.

Akizungumza mara baada ya kuanza kazi, Batarokota amesema anafuraha kupata heshima hiyo kubwa hivyo ataitendea haki nafasi hiyo.

Aidha batarokota amesema anatarajia kutambulisha singo nyingine mpya yenye miondoko ya asili.


Batarokota alitamba na wimbo wake wa Kwejaga-Nyangisha ambao ulimwezesha kuingia katika tuzo za Kill Music Award 2014 ambapo msanii Diamond Plutinumz alizoa tuzo saba.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI