RODGERS AFURAHISHWA NA SARE



Mwalimu Brendan Rodgers amesema Liverpool wanarejelea ubora wao baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya maadui wa jadi Everton katika uga wao wa Anfield Jumamosi.

Nahodha wao, Steven Gerrard, alifunga goli lake la 10 katika mechi 32 dhidi ya waasimu hao muda mfupi baada ya kugonga saa lakini kapteni mwenzake, Phil Jagielka, alifungulia kombora kali kunusuru timu yake katika muda wa majeraha.

Liverpool waliomaliza nafasi ya pili musimu uliopita wameshinda mechi mbili pekee muhula huu baada ya mechi sita na Rodgers alitangaza walistahili ushindi.


“Bila shaka, hatukupata kile tulifaa. Tulikuwa wazuri zaidi na kufungwa bao hilo ni ishara ya bahati mbaya. Lakini kwa juhudi, tunarudi mahala tulipokuwa miezi 19 iliyopita. Kiufundi, tuliweza kutawala na baada ya kuchukua uongozi, tulifaa kuongeza kuongezea goli moja ama mawaili,” Rodgers alinena.
“Ni jambo la kutamausha kufungwa bao jinsi hiyo,” aliongeza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA