KRISH FLAVOUR, MATONYA WAJA NA SHALABILEMA.
Msanii anayeibukia Omary Abdallah "Krish Flavour" ameibuka na ngoma matata 'Shalabilema' aliyomshirikisha mkali mwingine Seif Shaaban "Matonya" ambaye alipata kung'ara na nyimbo kadhaa.
Akizungumza na gazeti hili Flavour amesema ameamua kuimba wimbo huo na kumshirikisha Matonya ambaye naye ameonyesha uwezo wake, Flavor ametaja maana ya Shalabilema ni mwanamke msafi anayejipenda ikiwa na maana sawa na neno Sharobalo.
Flavour ameongeza kuwa muziki alianza tangia mwaka 2008 na aliachia wimbo wake wa kwanza uitwao 'namba moja' aliyomshirikisha Tanzanite na aliifanya katika studio ya Fire Music chini ya prodyuza more fire.
Mwaka 2000 wimbo huo wa 'Namba moja' ndio ulianza kupigwa katika vituo kadhaa vya redio, ameongeza kuwa hadi sasa amesharekodi nyimbo zaidi ya 14 lakini bado hajapata bahati ya kukubalika na kupata mafanikio kama ilivyo kwa wasanii wengine waliofanikiwa.
Ameongeza kuwa wimbo wake wa Shalabilema ambao amemshirikisha Matonya ameurekodi katika studio ya Paris Record chini yake Prodyuza Dav Dizo.
Kwa sasa anajiandaa kuachia ngoma nyingine mpya na ile video ya Shalabilema itakua hewani, Flavour ambaye ana mfadhili wake anayemwezesha kuingia studio ingawa amekataa kumweka hadharani.
aidha Flavour amewaomba mashabiki wake wajiandae kupokea radha tofauti kutoka kwake.