SIMBA YAREJEA DAR KUIVAA GOR MAHIA
Timu ya Simba inarudi jijini Dar es Salaam kesho kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, huku kocha Patrick Phiri akitarajia kuwatumia washambuliaji wake wapya wa kigeni Mkenya Raphael Kiongera na Mganda Emanuel Okwi.
Hata hivyo, Phiri atalazimika kumuanzisha mmoja kati yao ili acheze na Elias Maguli, ambaye atachukua nafasi ya Amissi Tambwe aliyekwenda kuichezea timu yake ya Taifa ya Burundi.
Washambuliaji wote hao wamechelewa kujiunga na kambi hiyo kwani Okwi ameingia dakika za mwisho za usajili akitokea Yanga, wakati Kiongera akiwa kwao kuisaidia timu yake ya zamani, KCB katika baadhi ya mechi ili isishuke daraja.
Katika mechi hiyo, Simba itawakosa wachezaji wake sita,ambao ni Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Said Ndemla, Joram Mgeveke, Pierre Kwizera pamoja na Tambwe watakaokuwa katika majukumu ya timu zao za taifa.
Akizungumza mara baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Chuoni Chukwani, Phiri alisema wachezaji walioondoka ni wengi hivyo anatakiwa kuumiza akili kupanga kikosi ambacho ni cha uhakika.
“Tutacheza na Gor Mahia, timu ambayo ni nzuri, wachezaji wengi wameondoka kwenda katika timu za Taifa, hadi sasa wameongezeka wengine kama Okwi na Kiongera,” alisema kocha huyo Mzambia.