PHIRI AJIVUNIA KIONGERA, OKWI,ATAMBA KUZISURUBU YANGA, AZAM

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Simba, Mzambia Patrick Phiri amesema uwezo alioonyesha mshambuliaji Raphael Kiongera (pichani), kwa kushirikiana na Emmanuel Okwi umekifanya kikosi chake kuwa imara katika safu ya ushambuliaji.

Kiongera na Okwi Jumamosi walionyesha ushirikiano mzuri kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya wakati Simba ikishinda 3-0.

Akizungumza juzi, Phiri alisema Kiongera ameonyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo na kuelewana vema na Okwi tofauti na alipocheza sambamba na Elias Maguri katika kipindi cha kwanza.

"Nilimuingiza Kiongera baada ya kuona Maguri na Okwi wanapoteana katika mchezo huo,"alisema Phiri. "Baada ya kuingia Kiongera safu ya ushambuliaji iliongezeka nguvu na kubadilika hivyo Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0."

Alisema Kiongera aliyechelewa kujiunga na wenzake katika kambi yao iliyokuwa visiwani Zanzibar ni tofauti na ya sasa kwa kuwa kuna vitu vilivyoongezeka kwake.

Mzambia huyo alisema hilo linampa matumaini ya timu yao kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara, inayotarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA