OKWI AWAAMBIA YANGA WATAFUNGA MDOMO TU.
Licha ya kupika mabao yote ya Simba katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu waliyotoka 2-2 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi, mshambuliaji Emmanuel Okwi amesema hakuwa katika kiwango chake.
Okwi, aliyejiunga na Simba dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili msimu huu akitoka Yanga, alisababisha mabao yote ya Simba juzi licha ya mashabiki wa Yanga kumzomea mwanzo mwisho jambo analoamini muda si mrefu watatulia baada ya kurejea katika makali yake.
Bao la kwanza la Simba lilipatikana baada ya Okwi kukwatuliwa nje ya mstari wa eneo la hatari la Coastal Union, hivyo adhabu hiyo kuzaa matunda kupitia kwa mpigaji Shabani Kisiga kabla ya Mganda huyo tena kutoa pasi ya mwisho ya bao la pili kwa mfungaji bora wa VPL msimu uliopita, Mrundi Amissi Tambwe.
Kisiga alifunga kwa 'frikiki' iliyomshinda kipa wa Coastal, Shaban Kado wakati mabao ya mabingwa hao wa Tanzania Bara 1988 yalifungwa na mtokea benchi Lutimba Yayo na mshambuliaji wa zamani wa Gor Mahia ya Ligi Kuu ya Kenya, Rama Salim.
Mara tu baada ya mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Jacob Adongo kutoka Mara kumalizika, Okwi aliliambia NIPASHE kuwa bado hajafikia katika kiwango chake cha kusakata soka.
“Mara nyingi sipendi kuzungumzia kiwango changu binafsi kuliko cha timu, tulicheza vizuri kipindi cha kwanza na Coastal walicheza vizuri kipindi cha pili,” alisema Okwi.
“Sijafurahishwa sana na kiwango nilichoonyesha leo (juzi), nitajitahidi kuongeza mazoezi ili mechi ijayo niisaidie timu yangu kupata ushindi,” alisema zaidi Mganda huyo ambaye muda wote wa mechi ya juzi alikuwa akizomewa na mashabiki wa Yanga waliokuwa wameingia uwanjani kutazama mechi hiyo.
Alipoulizwa juu ya zomea zomea inayofanywa na mashabiki wa Yanga dhidi yake, Okwi alisema: “Sina muda nao, mimi nimeshakuwa mchezaji halali wa Simba, mambo yote kuhusiana na Yanga hayanihusu.
Ninaamini nitakapokuwa katika kiwango changu, hawatanizomea tena,” alisema.
Okwi, mchezaji wa zamani wa SC Villa ya Ligi Kuu ya Uganda na Etoile du Sahel ya Tunisia, amejiunga na Simba baada ya uongozi wa Yanga kuwasilisha nyaraka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zikionyesha kuwa mkataba wake wa miaka miwili na nusu na klabu hiyo ya Jangwani aliousaini Desemba 13, mwaka jana, umevunjwa.