PHIRI AIPELEKA SIMBA RWANDA
Wakati kocha wa Simba, Patrick Phiri, akisema kikosi cha timu yake sasa ni sawa na 'moto usioshikika', timu hiyo inasaka wapinzani kutoka Rwanda baada ya kufutika kwa mechi yao iliyopaswa kuchezwa keshokutwa Jumatano dhidi ya Big Bullets kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana, Phiri, alisema kuwa kikosi chake kimeiva na kiko tayari kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayo itaanza Septemba 20 mwaka huu.
Phiri alisema kuwa kiwango kilichoonyeshwa na timu yake katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kilimfurahisha na kilikuwa cha juu.
Mzambia huyo mwenye rekodi ya kuipa Simba ubingwa wa Bara bila kufungwa katika msimu wa mwaka 2008/2009 alisema anaamini Simba itarejesha heshima waliyoipoteza miaka miwili iliyopita.
Alisema kwamba kila mchezaji anajituma kuonyesha kiwango chake ili kuisaidia timu na kuongeza kuwa ushindani wa namba ni mkubwa katika kikosi chake.
"Nina furaha na kiwango cha timu yangu, hii inaonyesha vijana wako tayari kwa ligi na hawana wasiwasi...Simba ni moto sasa," alisema Phiri.
Kocha huyo aliongeza kuwa baada ya jana kuwapa mapumziko wachezaji wake, leo timu hiyo itaingia kambini Kunduchi kuendelea na mazoezi.
Naye Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema jana kuwa uongozi umefurahishwa na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gor Mahia na kiwango cha timu kilivyoonyeshwa.
Aveva alisema kuwa baada ya mechi kuahirishwa kwa keshokutwa iliyokuwa dhidi ya Big Bullets, kikosi cha Simba kitasafiri kuelekea Mtwara kucheza mechi nyingine dhidi ya Ndanda FC katika kuadhimisha siku ya Ndanda Day.
Alisema timu itaondoka jijini Dar es Salaam Ijumaa na itakuwa ni nafasi nyingine ya kuwapima wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kuonekana katika mechi zilizotangulia.
Aliwashukuru na kuwaomba mashabiki na wanachama wa Simba kuendelea kujitokeza kuiangalia timu yao katika mechi za kirafiki wanazocheza ndani na nje ya Dar es Salaam.
Simba ilizifunga 2-1 Kilimani City, 2-0 Mafunzo na 5-0 KMKM, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar kabla ya juzi kuifumua 3-0 Gor Mahia.
Simba itaanza kampeni ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara msimu ujao kwa kuikaribisha Coastal Union Septemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini.