WAAMUZI ZANZIBAR KIMEELEWEKA

WAAMUZI 21 wanaochezesha soka visiwani Zanzibar wamefaulu katika mtihani wao wa utimamu wa mwili (Kopa Test) uliofanyika juzi visiwani Zanzibar.

Mtihani huo ambao ulikuwa chini ya wakufunzi Muhsini Ali Kamara na Juma Ali David kutoka Zanzibar na mkufunzi kutoka Dar Es Salaam Riziki Majala, ulishirikisha waamuzi 25.

Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa Soka Zanzibar (ZAFRA) Issa Ahmada Hija ‘Jogoo’ alisema kuwa waamuzi hao waliofaulu watachezesha ligi kuu ya Zanzibar pamoja na ligi daraja la kwanza na la pili Taifa.

Aidha akizungumzia waamuzi wanne ambao wamefeli waamuzi waliofeli mtihani huo watapewa nafasi ya kutahiniwa tena mara baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu kumalizika.


Mwenyekiti huyo amesisitiza waamuzi hao kuchezesha mechi kwa kufuata sheria 17 za Soka na kwamba bila hivyo watakuwa wanavunja kanuni za soka zilizowekwa na Shirikisho la Dunia la mchezo huo (FIFA).

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA