ALIYEMPIGA KICHWA MWAMUZI AENDA JELA

Ismail Gunduz
Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kuto cheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani mwamuzi wa mchezo.


Gunduz anayechezea timu ya daraja la tano ya SK RUM alimpiga mwamuzi siku ya Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo.
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kugongwa kichwa hicho.

Kwa mjibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa kosa kama hilo ni kufungiwa michezo 108.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA