Shearer asema Welbeck atang'ara Arsenal

Mshambuliaji mpya wa kilabu ya Arsenal Danny Welbeck anaweza kufunga mabao 25 kwa msimu mmoja ,hayo ni matamshi ya aliyekuwa mshambuliaji wa England Allan Shearer.

Wellbeck mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na kikosi cha The Gunners kutoka kilabu ya Manchester United kwa kitita cha pauni millioni 16 katika siku ya mwisho ya dirisha la kuwasajili wachezaji wa soka barani ulaya na anaweza kuanzishwa kwa mara ya kwanza dhidi ya watetezi wa ligi hiyo Manchester City siku ya jumamosi.

Nimesikia watu wakisema kwamba Wellbeck hawezi kufunga mabao 20 ama 25 kwa msimu mmoja ,sikubaliani na hilo Shearer aliiambia Radio 5 live ya BBC'',.

''Sasa ana uwezo wa kuonyesha umahiri wake katika ligi hiyo.''.

Siku ya Alhamisi Meneja wa kilabu ya Manchester United Van Gaal alisema kuwa Wellbeck hakuweza kufunga mabao ya kutosha wakati alipkuwa katika kilabu hiyo ya Old Trafford.

Mshambuliaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Manchester ambaye aliifunga mabao yote mawili timu ya Uingereza dhidi ya Switzerland siku ya jumatatu ,hajawahi kufunga zaidi ya mabao tisa katika ligi ya Uingereza tangu alipoanza kuchezea mwaka 2008.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA