WENGER AKIRI DORTMUND WALISTAHILI USHINDI

Arsene Wenger

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameungama kuwa timu yake ilitepetea na walistahili kichapo cha 2-0 walichopokea Ujerumani mikononi mwa Borussia Dortmund kwenye mechi ya ufunguzi ya ligi ya mabingwa Jumanne.

Ciro Immobile na Pierre-Emerick Aubameyang walipatia miamba hao wa Ujerumani alama zote tatu kwenye Kundi D kwenye uga wa Westfalenstadion baada ya wenyeji kulemea Arsenal kotoka kipenga cha kwanza.
Ingawa walikosa makali yao ya kawaida, wana Gunners walipoteza nafasi nadra walizozipata na mwishowe, mwalimu wao alikiri waliwezwa na timu bora zaidi.


“Hatukufikia kiwango kinachotakikana usiku wa leo. Walistahili ushindi wao. Juu ya hayo, tulikuwa na bahati mbaya kwani sekunde kumi kabla ya kufungwa la kwanza, mpira wa kurushwa ulikuwa wetu.

“Licha ya onyesho letu duni, tulikuwa na nafasi mingi na hilo ni sadfa. Walipata nafasi mingi pia lakini tulistahili kuongoza,” Wenger alinena.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA