WITNESS MWAIJAGA AKEMEA ULEVI KWA WASANII WAWAPO JUKWAANI

Na Robert Michael

MSANII wa kizazi kipya aliyepata kung'ara na kundi la Wakilisha lililokuwa likishirikisha nyota watatu Witness Mwaijaga amekasirishwa na kushushwa kwa hadhi ya muziki huo nchini na baadhi ya wanamuziki.

Mwanadada huyo mkali katika muziki wa miondoko ya Hiphop anaetamba na nyimbo zake ambazo ni "Zero" amemshirikisha Fid Q, "Safari" pamoja na "Attention", ambaye maskani yake ni Tukuyu mkoani Mbeya, amesema kuna baadhi ya wasanii wa Bongo wamekuwa wakishusha hadhi muziki wa Hiphop.


Akizungumza kwa njia ya simu Witnnes amesema kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakifanya shoo wakiwa wamekunywa pombe wakidai kuwa pombe inawapa Mzuka kwenye shoo, matokeo yake pombe inasababisha kufanya mambo yasiyofaa kwenye jukwaa.

Witness ameuambia mtandao huu kuwa asilimia kubwa wasanii wa kibongo wamekuwa hawana nidhamu wanafanya mziki kutokana na fulani amefanya mziki au kwa lengo la kupata Wanawake/wanaume.

Hivyo amewataka wasanii wenye tabia hizo wabadilike na wafanye muziki kulingana na maadili ya kitanzania, Witnnes aliibukia kwenye kundi la Wakilisha lililotokana na shindano ya Tusker Project Award ambapo yeye na wenzake Shaa na marehemu Langa walishinda.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA