RIO FERDINAND ALIVYOTEMWA 'KIROHO MBAYA' MAN UNITED
BEKI Rio Ferdinand amemaliza maisha take ya soka Manchester United baada ya kuambiwa hatapewa Mkataba mpya.
Mkuu
wa Old Trafford, Ed Woodward alimpa habari hizo za kusikitisha
Ferdinand mwenye umri wa miaka 35 katika chumba cha kubadilishia nguo
Jumapili wakati wa mchezo wa mwisho na Southampton.
Wengi
wamesikitishwa na kitendo cha Woodward kuamua kumuacha 'kiroho mbaya'
Ferdinand baada ya miaka 12 ya kuitumikia klabu hiyo kwa moyo wake wote.
Kumbukumbu
za furaha: Ferdinand akiwa ameshika taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
mwaka 2008 na Cristiano Ronaldo baada ya kuifunga Chelsea kwa penalti
Alipowasili:
Ferdinand akikabidhiwa jezi ya United na mocha wakati huo, Sir Alex
Ferguson baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Leeds kwa dau la
uhamisho la Pauni Milioni 29.1 Julai mwaka 2002
FERDINAND MAN UNITED
Kusajiliwa: July 2, 2002
Ada: Pauni Milioni 29.1
Mechi alizocheza: 455
Mabao aliyofunga: 8
Mataji aliyoshinda: Ligi
Kuu (2002/03, 2006/07, 2007/08, 2008/09, 2010/11, 2012/13), Ligi ya
Mabingwa (2007/08), Kombe la Ligi (2005/06, 2008/09), Kombe la Dunia la
Klabu (2008)
Katika
taarifa aliyoweka kwenye tovuti yake binafsi usiku wa jana, Ferdinand
amesema; "Mambo fulani yamenifanya nishindwe kusema kwaheri kwa namna
amabyo ningependa,".
Na
huku akiwa amekubali kumruhusu beki mwingine wa kati Nemanja Vidic
kuondoka, mchezaji mwenzake wa zamani Ferdinand, Gary Neville ametweet:
"Hivyo inaonekana kama Rio na Vida wameruhusiwa kuondoka!!!
Beki
huyo wa zamani wa England amewaambia wenzake safe ya 1-1 juzi ndiyo
ilikuwa mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo wakiwa kwenye ndege
kurejea kutoka St Mary na akawaomba wamsainie mpira abaki nao kama
kumbukumbu yake.
Ferdinand,
ambaye alikuwa mchezaji ghali kihistoria England wakati anasajiliwa
United kutoka Leeds kwa dau la Pauni Milioni 29.1 Julai mwaka 2002,
ameichezea timu hiyo mechi 455 lakini alionekana hafai chini ya David
Moyes.
Amemwaga
damu: Ferdinand akisindikizwa kutoka uwanjani na Robin van Persie baada
ya kuchanwa na sarafu iliyorushwa uwanjani na mashabiki wakati wa mechi
ya mahasimu wa Jiji la Manchester mwaka 2012
Alikuwa anafunga pia: Ferdinand akifunga boa dhidi ya Liverpool katika ushindi wa 2-0 Uwanja wa Old Trafford mwaka 2006