Q CHILLA ATOBOA KILICHOMUUA KUAMBIANA

Na Robert Michael

Msanii huyo wa "Bongo Fleva" akizungumza na blog hii amesema kifo cha "Adam Kuambiana" kilimkuta akiwa kwenye kambi ya kurekodi "Filamu".

Wakiwa wanajitayarisha "Jumamosi" waanze kushuti filamu ya Adam Kuambiana inayoitwa "Jojo".Q Chillah anasema siku ya Ijumaa jioni Kuambiana" na wasanii wenzake walikuwa "Baa" wakinywa pombe.

Hadi usiku wa Saa 8, Lakini Kuambiana alikunywa pombe huku akidai tumbo linamsumbua,Baada ya kumaliza kila mmoja alikwenda kulala.Ilipofika kesho yake "Jumamosi" saa 3.00.


Msanii "Kuambiana" hali yake ilikuwa sio nzuri kisha alikwenda chooni na akajikuta akiendesha damu hivyo nguvu zilimuishia ndipo "Q chillah" na wasanii wenzake walimpeleka hospitali ya Mama ngoma iliyopo Mwenge Jijini Dar es salaam akalazwa muda mfupi katika hospitali hiyo kisha akafariki dunia.

Pamoja na hayo Q Chillah ameongeza kwa kusema kuwa Kuambiana ndie alie mshawishi aingie kwenye tasnia ya Uigizaji.

Marehemu Kuambiana alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jirani kabisa alipozikwa Steven Kanumba,

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA