DIDA AAMUA KUACHANA NA YANGA, HUENDA AKATIMKIA UARABUNI.
Kipa chaguo la kwanza kwa Yanga kwa sasa Deogratius Munishi 'Dida' amesema hana uhakika wa kuendelea kubaki Yanga baada ya mkataba wake kumalizika kutokana na kasumba iliyoibuka ya kutokuwa na imani na wachezaji pindi timu inapokuwa na matokeo mabovu.
Akizungumza na Mtandao huu akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa (Taifa Stas) iliyopo Tukuyu jijini Mbeya jana, Dida aliyejiunga na Yanga mwaka jana akitokea Azam FC, alisema hana uhakika wa kuendelea kuvaa uzi wa njano na kijani wa Yanga baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika.
"Kwa sasa bado nina mwaka mmoja wa kuitumikia Yanga lakini baada ya hapo sijui nitakakokuwa. Nitakuwa katika kipindi kizuri zaidi cha kuzungumzia hatma yangu baada ya kumalizika kwa mkataba," alisema Dida na kuongeza:
"Kuna mambo mengi yanayojiri ndani ya klabu na sina uhakika kama Wanayanga watakuwa na hamu na mimi baada ya msimu ujao maana ukiharibu mara moja wanakuhukumu na kusahau mazuri yote uliyofanya."
Dida, akiwa ni mchezaji huru baada ya kumalizana na Azam FC waliomsimamisha kwa tuhuma za rushwa msimu wa 2012/13, alijiunga na Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili Juni 27 mwaka jana kwa mapendekezo ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mholanzi Ernie Brandts.
Hata hivyo, kipa huyo alilazimika kusugua benchi kwa muda mrefu hadi kipa mwenzake Ali Mustafa 'Barthez' alipoharibu baada ya kufungwa magoli matatu katika sare ya maajabu ya 3-3 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 20 mwaka jana.
Dida amejihakikishia namba katika kikosi cha kwanza cha Yanga baada ya kipa mkongwe Juma Kaseja aliyesajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo la usajili msimu huu kujikuta akifungwa magoli ambayo Wanajangwani waliyatafsiri ya kizembe na kuamua kumweka kando.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 25 pia ni mlinda mlango chaguo la kwanza kwa benchi la ufundi la Stars. Aishi Manula wa Azam FC ndiye kipa chaguo la pili kwa benchi hilo linaloongozwa na kocha mpya Mholanzi Mart Nooij.