MUZIKI NI ZAIDI YA SOKA- HAMOSNOTA

Na Mariamu Libibo

MSANII chipukizi wa miondoko ya kizazi kipya anayetamba na wimbo wake wa 'Bye bye' Hashim Momba 'Hamosnota' (Pichani) amedai muziki ni zaidi ya mchezo wa soka na kama serikali ingetambua hilo ingewekeza vya kutosha.

Akizungumza katika ofisi za Mambo uwanjani blogspot Hamosnota amesema anashangazwa na serikali kung'ang'ania mchezo wa soka ambao umeshindwa kuipa heshima nchi wala kuingiza mapato ya kutosha.

Ameongeza kuwa kama serikali ingetumia muziki basi ingenufaika kwani unaingiza fedha nyingi kuliko soka, ametolea mfano shoo ya mwanamuziki Diamond Platinum iliyofanyika mwaka jana Mlimani City ambapo kiingilio chake ilikuwa 50, 000 na tiketi zilikwisha.

Pia amedai kwenye shoo za muziki hakuna wiz\i kama ilivyo kwenye soka ambapo wizi wa tiketi umekuwa wimbo wa taifa, 'Serikali ingetumia muziki ingenufaika sana kwani muziki ni sehemu ya burudani kwa kiola mtu hivyo huingioza fedha nyingi', aliendelea.


'Hata hivyo serikali imenufaika sana kupitia muziki kwani imekusanya fedha nyingi katika matamasha mbalimbali' alisema, Aidha Hamosnota amedai mafanikio ya msanii Diamond Platinum yamedhihirisha kuwa muziki umepiga hatua kubwa kuliko soka.

'Diamond Platinum ameitangaza Tanzania kimataifa, kwani ameingia kwenye tuzo kubwa kama vile ya Afrika inayodhaminiwa na MTV pamoja na ile ya BET inayofanyika nchini Marekani, najua Diamond atakutana na mastaa mbalimbali wa duniani ambao nao wamo katika tuzo hizo, alisema chipukizi huyo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA