PAZIA LA USAJILI KUFUNGULIWA JUNI 15
Dirisha la usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara 2014/2015 unatarajiwa kuanza Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu, imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana, Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa klabu zinatakiwa kuzingatia muda huo uliopangwa ili kuepusha malalamiko kutoka kwa wachezaji wao.
Wambura alisema kuwa klabu zinatakiwa kutangaza kuacha au kusitisha mikataba yao kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu wakati kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu.
Alisema kuwa kamati husika itakutana na kupitia majina na kutangaza pingamizi zitakazokuwa zimewasilishwa kati ya Agosti 4 na 11 mwaka huu wakati uthibitisho wa usajili hatua ya awali ni Agosti 12 hadi 14 mwaka huu.
Alieleza kwamba usajili wa hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 14 na 29 mwaka huu na muda wa kupitia na kutangaza majina ya pingamizi ya hatua ya pili ya usajili huo utaanzia Agosti 30 hadi Septemba 4 mwaka huu.
" Uthibitisho wa usajili hatua ya pili umepangwa kuwa kati ya Septemba 5 na 6 mwaka huu", Wambura alisema.