MSHIRIKI WA KTMA 2014 AKUTWA KWA SANGOMA MWANZA
Na Saida Hoza- Mwanza
ALIYEKUWA mshiriki wa Kili Music Award 2014 Batarokota Linda amenaswa na kamera yetu akiwa kwa sangoma yaani mganga wa kienyeji akipatiwa dawa.
Mwandishi wetu ambaye amepiga kambi jijini Mwanza ametabaisha kuwa mwanamuziki huyo wa nyimbo za asili amekuwa na kawaida ya kufuata dawa kwa sangoma huyo.
Chanzo chetu cha habari kinaamini Batarokota amefuata ndumba ili afanye vizuri na kunyakua tuzo mbalimbali mwakani.
Msanii huyo alipozungumza na Mtandao huu kuhusu kukutwa kwake kwa sangoma huyo, amekiri kutumia dawa za kienyeji lakini amekataa kuhusisha na imani za kishirikina.
Aidha amefafanua kuwa sangoma huyo ni babu yake na amekuwa akimsaidia mara kwa mara, kuhusu kufuata dawa: Batarokota amesema ni kweli amekuwa akisumbuliwa kwa muda na mrefu na ugonjwa wa kichomi.
'Yule ni babu yangu na siwezi kumtenga na amekuwa akinipa dawa za kichomi ambacho kikinitesa sana niwapo jukwaani;, alisema na kuongeza.
'Mimi ni mkristo safi tena Katoliki namwamini Yesu, ila dawa za mitishamba naziamini sana na zilikuwemo tangia enzi za kale kabla ya kugundulika teknolojia', alisema.
Batarokota aliingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za KTMA 2014 na wimbo wake wa kisukuma Kwejaga-nyangisha