CD YA JAY-Z AKICHAPWA NA WIFI YAZUA BALAA
Mitandao ya kijamii imewaka moto
kufuatia kanda ya video iliyozuka ikionyesha dadake mwanamuziki wa
kimataifa Beyonce Knowles , Solange Knowles akimchapa makonde
mwanamuziki Jay-Z ambaye pia ni shemeji yake katika lifti.
Hata hivyo kanda hiyo haikuwa na sauti bali ilionyesha tu kitendo cha dadake Beyonce akimpacha Jay-Z na hata kujaribu kumpiga teke mara mbili wakiwa ndani ya lifti hiyo pamoja na Beyonce na mlinzi mmoja wa Jay-Z aliyejaribu kumzuia Solange.
Kanda hiyo ilizuka baada ya Beyonce aliyekuwa ameambatana na mumewe Jay Z pamoja na Solange kuhudhuria tamasha la kifahari mjini New York tarehe tano Mei.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, taarifa kutoka kwa maafisa wa hoteli ambamo kisanga hicho kilitokea walielezea kukasirishwa na mtu ambaye aliisambaza kanda hiyo kwenye internet na hata kutishia kumchukulia hatua pindi atakapojulikana.
"tumeshtushwa sana na kukasirishwa na mtu aliyekiuka sheria zetu za faragha ambazo wageni wetu wanathamini sana, '' ilisema taarifa kutoka kwa wakuu wa hoteli hiyo.
"tunachunguza hali hiyo na pia yeyote atakayepatikana na hatia ataadhibiwa vikali.''
Wasimamizi wa Beyonce walikataa kuzingumzia kisa hicho.