TP MAZEMBE YAENDELEZA MAUAJI TENA
TP Mazembe walishindi mahasidi
wao wa jadi AS Vita kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo katika mechi
iliyobashiriwa kuwa ngumu ya kundi A ya kuwania ubingwa wa Afrika
miongoni mwa vilabu .
Kufikia sasa timu zote zilizo katika kundi A zimeshinda mechi moja moja baada ya klabu ya Misri, Zamalek, kuishinda Al Hilal ya Sudan jijini Kairo na kunyakua pointi 3.
Ahly iliilaza Esperance ingawa walipoteza kwa kutocheza mechi yao ya nyumbani kufuatia machafuko ya wafanyikazi katika mji upatikanao katika pwani ya Tunisia, Sfax.