MAN CITY YAMWANGUKIA YAYA TOURE

MKURUGENZI wa soka wa Manchester City, Txiki Begiristain atafanya mazungumzo ya amani na Yaya Toure kabla ya kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia ili kumaliza tofauti zilizojitokeza kati ya kiungo huyo na klabu hiyo.


Wakala wa Toure, Dimitry Seluk aliibua mjada;la mzito Jumanne baada ya kusema mchezaji huyo anawezankuondoka kwa klabu hiyonimeonyesha haimjali baada ya kupuuza shsrehe za siku yake ya kuzaliwa.

Alisema mmiliki wa mabingwa hao wa Ligi Kuu England, Sheik Mansour hakuonyesha jitihada za kutosha katika sherehe za miaka 31 ya kuzaliwa MwansokanBora Afrika wakati timu hiyo ilipofaya ziara Abu Dhabi wiki iliyopita.

Kuna fikra kwamba Seluk anajaribu kufanya mpango wa kumrejesha Barcelona mchezaji huyo aliyeondoka Nou Camp kwa dau la Pauni Milioni 24 mwaka 2010.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA