HAPANA CHEZEA MBEYA CITY WEWE! YATINGA ROBO FAINALI SUDAN

MBEYA City imetinga Robo Fainali za michuano ya Nile Basin inayoendelea nchini Sudan kufuatia sare ya bila kufungana na Enticelles ya Rwanda usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Khartoum.

Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City imalize na pointi nne baada ya mechi tatu, ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya AFC Leopards ya Kenya walioongoza kundi kwa pointi zao tisa.

Enticelles imemaliza nafasi ya pili kwa pointi zake mbili na Academie Tchite ya Burudi imemaliza mkiani mwa Kundi B kwa pointi moja iliyovuna kwenye sare na timu ya Rwanda.


Katika mchezo mwingine wa kundi hilo michuano hiyo inayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA au washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leopard imeifunga Tchite 1-0.

Bao pekee la Ingwe limefungwa na kiungo wa zamani wa Simba SC ya Tanzania, Mganda Mussa Mudde, ambalo hilo linakuwa bao lake la pili kwenye michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, baada ya awali kuwafunga Mbeya City, Leopards ikishinda 2-1.

Mbeya City na AFC Leopards sasa zinasubiri kujua wapinzani wao katika Robo Faibali baada ya mechi za mwisho kesho usiku.

Mbeya City; David Burhan, Yussuf Abdallah, Hamadi Kibopile, Christian Sembuli, Yohanna Morris, Athony Matogolo, Deus Kaseke, Steven Mazanda, Paul Nonga, Mwagane Yeya na Themi Felix.

Enticelles; Nsanganira Djuma, Ndayisenga Mbanyi,
Hategekimana Abdallah, Nkusi Prince, Nahimana Isiyaka, Gasangwa Salum, Ndikumasabo Ibrahim, Ismail Mugabo, Manishimwe Yves, Arafat Bahame na Herorimana Bosco.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA