Ruka hadi kwenye maudhui makuu

YAYA TOURE ATHIBITISHA KAULI YA WAKALA WAKE, SASA KUHAMA RASMI MAN CITY

MWANASOKA bora wa Afrika, Yaya Toure ameibuka kumsapoti wakala wake, Dimitri Seluk aliyeishambulia Manchester City kwa kutojali kuhusu birthday ya kiungo huyo.

Yaya amesema yote aliyoyasema Seluk ni ukweli mtupu na yeye ataamua mustakabali wake baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao.

Seluk ameelezea shaka ya mchezaji huyo wa Ivory Coast kubaki Etihad kwa kusema kiungo huyo tegemeo haifurahii na klabu hiyo.


Na Toure ametweet: "Wakala wangu alikuwa anajaribu kuelezea ukweli kwa niaba yangu, utani pembeni. Inasemekana muhimu kwangu ni kutoa taarifa.. Nitafanya hivyo. Kila kitu alichosema Dimitry ni ukweli. Amenizungumzia.

Nitatoa mahojiano ya kufafanua baada ya Kombe la Dunia,".
Amekasirishwa: Yaya Toure amekasirishwa na kitendo cha Manchester kutojali kuhusu sherehe yake ya kuzaliwa

Kiungo huyo wa Ivory Coast, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake unaomfanya alipwe Pauni 220,000 kwa wiki, imeelezwa amechukiwa na kitendo cha kutotumiwa salamu za kufurahia miaka 31 ya kuzaliwa kwake.

Wakala wa Toure, Dimitri Seluk amesema: "Kuna uwezekano mkubwa Yaya akaondoka majira haya ya joto. Amechukizwa. Kilichotokea katika birthday take kinamaanisha klabu haimjali. Imethibitika,"amesema.

"Wanaweza kusema vyovyote watakavyo, Oh tunampenda lakini tulisahau. Kusahau? Kuhusu Yaya? Mchezaji ambaye amekufanya umeshinda mataji mawili ya Ligi Kuu? Kijana ambaye amekusaidia kushinda Kombe la FA na Kombe la Ligi?

"Katika timu ya kawaida, wachezaji wenzake na klabu angalau wangempa salami za kumtakia heri. Lakini wakati umeshinda taji na siku mbili baadaye una pati kubwa kusherehekea taji na hakuna mtu aliyekwenda kumtakia happy birthday Yaya, nini zaidi unachotaka?

"Ikiwa mchezaji kama Yaya anakwenda Liverpool nawanashinda ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 24, Yaya atakuwa mzuri Liverpool,"alisema Seluk.

Amemtolea mfano beki wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Roberto Carlos alipewa gari aina ya Bugatti Veyron wakati wa birthday yake na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa