STAMINA ASHINDWA KUELEWANA NA MABEST.

Na Robert Michael

Wasanii hawa wa muziki wa Hiphop wameshindwa kuelewana kutokana na nyota wa music wa hiphop"Stamina" kutohudhuria kwenye shoe aliyoshirikishwa na msanii mwenzake "Mabest".

Inasemekana kuwa "Stamina" hakutoa taarifa ya kutoshiriki kwenye shoo hiyo kutokana na matatizo yake ya kifamilia.

Hali hii ilipelekea msanii "Mabest" kuchukizwa na kitendo hicho na kujikuta akimfokea na kumlaumu "Stamina" kuwa kitendo alichokifanya sio kizuri.

Aidha msanii "Mabest" aliona kuwa "Stamina" alifanya makusudi kutofika kwenye shoo yake. "Stamina" Anaiambia Blog hii kama ifuatavyo "Ndugu mwandishi sikuweza kumpa taarifa "Mabest" kwa sababu nilivurugwa na matatizo yaliyo tokea katika familia yangu hivyo "Mabest" nilimwelezea akutaka kunielewa.


'Mabest anathamini pesa kuliko afya ya mtu, Pesa anaweza kunilipa lakini afya ya familia yangu awezi kunilipa", Hali hii ilipelekea wasanii hawa kutoelewana na kufikia hatua ya kutowasiliana.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI