SEVILLA WAPELEKA TAJI LINGINE LA ULAYA HISPANIA

SEVILLA ya Hispania imetwaa ubingwa wa Europa League baada ya kuifunga Benfica ya Ureno kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.

Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Juventus, mjini Torino, Italia ulikuwa wa kawaida na timu zote zilicheza kwa tahadhari, hali iliyosababisha hata mashambulizi yawe machache.

Sifa zimuendee kipa Mreno wa Sevilla Antonio Alberto Bastos Pimparel aliyewazuilia ndugu zake leo na kucheza penalti moja ya Rodrigo, wakati ya Cardozo ilikwenda nje.


Ushindi wa Sevilla unamaanisha mataji yote ya klabu ya UEFA msimu huu yamebaki Hispania, kwani Atletico Madrid na Real Madrid nazo zitakutana katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa baadaye mwezi huu nchini Ureno.

Vikosi vilikuwa, Sevilla: Beto, Coke, Pareja, Fazio, Moreno, Mbia, Carrico, Reyes/Marin dk78/Gameiro dk104, Rakitic, Vitolo/Diogo Figueiras dk110 na Bacca.

Benfica: Oblak, Maxi Pereira, Luisao, Garay, Siqueira/Cardozo dk99, Ruben Amorim, Gomes, Gaitan/Ivan Calvaleiro dk119, Sulejmani/Andre Almeida dk25, Lima na Rodrigo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA