Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BRENDAN RODGERS AENDELEA KUULA LIVERPOOL

Brendan Rodgers ametia sahihi kandarasi mpya ya muda mrefu kuwa mkufunzi wa timu ya Liverpool iliyomaliza yapili msimu uliopita.


Rodgers ambaye alichukua usukani mwaka wa 2012 kutoka kwake Kenny Dalglish ameiongoza timu hiyo kushiriki ligi ya vilabu bingwa baada ya kukosa kushiriki ligi hiyo kwa miaka minne.

Rodgers

"‘Nimefurahi sana kufanikisha msingi ambao tumekuwa tukijenga kwa miaka miwili iliyopita,Sasa tunakwenda katika hatua ya pili ambayo naamini itakuwa ya kusisimua,na yenye kutuza."
Raiya huyo wa Ireland mwenye umri wa miaka 41 amesema kuwa anajihisi mwenye bahati kwa fursa hiyo ya kuongeza kandarasi na kusalia katika klabu hiyo.

Liverpool ilimaliza ya pili ikiwa na pointi mbili pekee nyuma ya mabingwa Manchester City katika msimu uliokamilika.

Timu hiyo ambayo imewahi kushinda ligi ya premia mara 18 ilikuwa na nafasi nzuri ya kunyakua taji hilo tena tangu mwaka wa 1990, kabla ya kulazwa mabao 2-0 na Chelsea matokeo yaliyoiruhusu mabingwa wa ligiu kuu ya Uingereza Manchester City kuipiku kileleni.

The Reds walikuwa wakiongoza kwa pointi tano walipoialika Chelsea mnamo tarehe 27 mwezi Aprili, lakini kushindwa kwao kukawafanya kupoteza kasi huku City wakishinda mechi zao zote zilizokuwa zimesalia na kumaliza wa kwanza.

John Henry

"Msimu huu umedhibitishia imani ya kila mmoja kwamba tunaweza kuleta mafanikio ya kandanda Liverpool na tunajitolea kufanya kazi pamoja kutimiza hilo."
Ijapokuwa taji la premia lilimponyoka Rodgers alitajwa kama mkufunzi wa mwaka na shirikisho la makocha wa ligi.

Mwenye hisa mkuu wa Liverpool John Henry na mwenyekiti Tom Werner, katika ripoti ya pamoja walisema kuwa klabu hiyo ya Anfield ilikuwa yenye ‘bahati sana’ kuwa na Rodgers kwenye usukani.
Mwanabiashara huyo wa Marekani alisema kuwa waliweka Imani yao kwa Rodgers kuweza kufanikisha azma ya klabu hiyo, huku akiongezea kuwa Rodgers ni kiungo muhimu sana kwa kile ambacho umiliki wa klabu hiyo kinajaribu kuafikia uwanjani.

John HenryJohn Henry
Henry alikamilisha ununzi wa Liverpool kwa Euro milioni 300 kutoka kwa mmarekani mwenzake Tom Hicks pamoja na Shirika la Marekani la Mill Financial mwezi Octoba 2010

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa