PROFESA J AWAPA SOMO WATU WENYE TABIA ZA UMBEA.

Na Robert Michael

Msanii mkongwe wa miondoko ya kizazikipya nchini Joseph Haule ' Profesa J' amewataka baadhi ya "Watanzania" waache kumsema vibaya kutokana na ukimya wake ama anapopata matatizo kwani kuna wakati binadamu anakuwa katika kkwamo wa kimaisha..

Profesa akireport katika blog hii amesema kuwa ameamua kufanya wimbo wake wa "Kipi sijasikia" alio mshirikisha "Diamond Plutnumz" msanii aliepata tuzo 7 za "Kili music award" ili kufikisha ujumbe kwa watu wanao mtakia mabaya pamoja na kuwaelimisha waache tabia hiyo ya umbea.

Aidha msanii huyo amesema kuwa kuna siku aliugua "Maralia" hivyo basi kutokana na kuugua alikonda lakini baadhi ya watu walisambaza umbea kuwa alikonda kwa "Ukimwi".


Vile vile "Profesa" amesema kuna kipindi alipotea kwenye game hivyo watu walidai kuwa amekufa.

Aidha "Rapper" huyo amesema pindi anarekodi wimbo wake wa "Kipi sijasikia", msanii "Diamond plutnumz" aliimba huku akidondosha machozi kutokana na kuguswa na ujumbe wa nyimbo hiyo ya "Kipi sijasikia".Pamoja na hayo "Profesa" ameongeza kwa kusema mziki wa sasa una tofauti kubwa na mziki wa zamani kama vile zamani kulikuwa na uhaba wa vifaa vya music.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA