MWANAMKE WA MIAKA 22 MBARONI KWA KUUZA MTOTO.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 Chinelo Huma amekamatwa na kitengo cha kupambana na biashara haramu ya kuuza binadamu cha jimbo la Enugu kwa kitendo cha kumuuuza mtoto wake mwenye umri wa mwezi mmoja .


Alikamatwa yeye pamoja na wanawake wenzake watatu Nkenchi Ugochukwu,Maria Asomba na Esther Obi ambao wanadaiwa kuhusika na kuuzwa kwa mtoto huyo.

Kamishna wa Polisi wa jimbo la Enugu Bw Mohammed Adamu ambaye alieleza wazi kwamba msichana huyo alipata ujauzito akiwa katika shughuri haramu za ukahaba.

Kamishna huyo alieleza kuwa Bi Ugochukwu (43)ambaye alinunua mtoto huyoinasadikika kwamba alikuwa anatamani kuwa na mtoto kwa muda mrefu ila kutokana na kushindwa kubeba mimba hali hiyo ilimpelekea kununua mtoto kwa kahaba huyo.

Bi Asomba (35) anashutumiwa kwa kosa la kuwashawishi wanawake wajawazito kuuza watoto zao endapo wakijifungua salama.Aidha Ugochukwu mnunuzi wa mtoto alisita kumkabidhi mtoto sababu aliwadanganya majirani zake kwamba mtoto mtoto
 aliyemnunua alijifungua.

Mama huyo ambaye alimnunua mtoto alikwisha mpa jina la Chinasa alieleza maumivu aliyoyapata baada ya kutokea tukio hilo pia alidai kuwa nilikuwa tasa kwa miaka mingi na ninahitaji mtoto,vile vile mume wangu amekuwa akinidhihaki sababu ya kutopata mtoto.

‘Huyu mtoto nilikabidhiwa April 17 2014 tukio hilo lilifanya nipongezwe na majirani zangu ila cha kushangaza mapolisi walikuja na kuniadhiri baada ya kumchukua mtoto na kutoboa siri kwamba hakuwa wangu’.

Alisema Ugochukwu
‘Mimi sihitaji pesa yangu shida yangu ni mtoto pia sikuwa na nia mbaya na huyu mtoto na nilikuwa nimeshajipanga kumpeleka kanisani mtoto huyu kwa aajili ya ubatizo’Aliongeza mnunuzi huyo wa mtoto.

Tatizo la kuuzwa kwa watoto limekuwa likikithiri sehemu nyingi sana Nigeria ni nchi inayokumbwa na baadhi ya wanawake wanaojifungua watoto na kuwauza.

Vyombo vya dola vinamkakati wa kutokomeza swala hili na watu wanaohusika na biashara hii haramu ni wale wanawake ambao ni wauza miili na wanafunzi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA