JK AWAREJESHA STARS SAMATTA NA ULIMWENGU
BAHATI ya aina yake. Washambuliaji wawili wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watawasili Jumamosi mchana kwa ajili ya kuichezea Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika Morocco mwaka 2015.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amesema kwamba, amewasiliana na Mwenyekiti wa TP Mazembe, Moise Katumbi na amemuhakikishia Samatta na Uli watatua Dar es Salaam Jumamosi.
Awali, ilikuwa wachezaji hao wasije kabisa kwenye mechi hiyo kwa sababu klabu yao inawahitaji kwa mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Lakini kwa kuwa mchezo wa kwanza wa Kundi lao, A dhidi yao na El Hilal Omduran utachezwa Ijumaa mjini Khartoum nchini Sudan, Jumamosi wachezaji hao watapanda ndege kuja Dar es Salaam na kucheza mechi Jumapili Uwanja wa Taifa.
Mara tu baada ya mwchi hiyo, wachezaji hao waterejea Lubumbashi DRC kwa maandalizi ya mchezo wa pili wa kundi lao dhidi ya AS Vita Mei 25, mwaka huu na baada ya hapo wanaweza kupata fursa ya kuja kwenda Zimbabwe kuchezea Stars mchezo wa marudiano.
Wazi kuja kwa wachezaji hao kuichezea Stars kunaongeza matumaini ya Stars kufanya vizuri, kwani Samatta na Ulimwengu kwa sasa ndio tegemeo la Tanzania.
Mshindi wa jumla kati ya Stars na Zimbabwe baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini, atapambana na mshindi kati ya Sudan Kusini na Msumbiji kuwania kuingia katika Kundi, rasmi kuanza mbio za Morocco 2015.
Chanzo Bin Zubeiry blog