AMINA NGALUMA KUZIKWA MCHANA HUU

Na Robert Michael

Mwanamuziki wa zamani wa kundi la African Revolutional 'Wana Tam Tam' pamoja na Double M Sound Amina Ngaluma 'Japaness' aliyefariki majuma mawili yaliyopita huko nchini Thailand anatarajia kuzikwa mchana huu katika makaburi ya Kitunda Machimbo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Muumini Mwinjuma 'Kocha wa Dunia'ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa bedni hizo zote zlizopitia marehemu Ngaluma, amedai kuwa mwanamuziki huyo anazikwa mchana katika makaburi ya Kitunda na umati mkubwa wa wakazi wa jiji laDar es Salaam watakitojikeza.

Mbali na wakazi wa Dar es Salaam, marehemu Ngaluma aliyetamba na wimbo wa 'Mgumba' atapata watu wqengi watakaokwenda kujitokeza kumzika, marehemu Ngaluma alifariki dunia nchini Thailand majuma mawili yaliyopita na mwili wake uliwasili nchini jana usiku.


Kabla ya umauti Ngaluma alikuwa kiongozi wa bendi ya Watanzania waliokuwa wakipiga muziki wao nchini Thailand, marehemu ameacha mume ila hakubahatika kupata mtoto, mungu ailaze roho ya marehemu Ngaluma mahara pema peponi_Aamina.

Wakati huo huo bodi ya ukurugenzi ya Mambo Uwanjani Publishers inatoa pole kwa wafiwa na kuwataka kuwa wavumulivu katika kipindi hikicha majonzi, jina la bwana lihimidiwe

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA