BAADA YA KUFUNGWA NA REAL MADRID, ATLETICO YAZUIWA NYOTA WAKE WOTE KUHAMA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjLr83jmkJs8jKtvdJhHmsgkMAQwtQp2KyaBePCfbyxxsLJUuMIGaeekLlGN4IuhuuCDcwVRqQ1Kw1JLDyGRyLgN5dXCEIQKDTofcrOZJRcJWKYwz3-bCdZemgjboQrgVmmp93av48u6pE/s1600/thibaut.jpg)
Kipa wa Chelsea anayecheza kwao kwa mkopo, Thibaut Courtois amezungumzia mustakabali wake baada ya kufungwa Real Madrid 4-1 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kwa kiasi kikubwa hayuko mikononi mwa Atletico.
"Sina mawasiliano ya moja kwa moja na Chelsea,"amesema kipa huyo mwenye umri wa miaka 22, Courtois. "Sina lolote dhidi yao. Ni kwamba nina dhamana hii na Atletico, baada ya yote nimeishi na klabu hii kwa misimu mitatu iliyopita,".
"Ikiwa nitatakiwa kurudi Chelsea tu kwa ajili ya kucheza mechi za Kombe la FA na Kombe la Ligi, nitaangalia mazingira," amesema.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhv1BkeN2JF2ZkOrELtdYeP8-_gQW2_hNb_KnqVCYpyewfSs830K8gKCA1II5dPpNXjyDrCNL0L0Ipx6eNivUZkdCoEYllUFOup9M2t7bIHEU1-qc3Q_L2uNxCOpCfkxGWoDGoGT1hgvk/s1600/COSTA+DIEGO.jpg)
Gil amesema: "Tutajaribu kuhakikisha kwamba wachezaji wore muhimu wanabaki hapa. Tumezungumza vizuri sana na Diego abaci na tunataka kutimiza ndoto hii, lakini itategemea na yeye mwenyewe,".
"Lengo letu ni kutouza mchezaji yeyote labda yule ambaye ataomba mwenyewe kuuzwa. Kwa sababu ya mafanikio yeti katika Ligi ya Mabingwa, tuna fedha maana yake hatuhitaji kuuza mchezaji,"amesema.
Kiungo Koke na beki wa kushoto, Filipe Luis ni wachezaji winging wanaozitoa udenda klabu za Ligi Kuu ya England.
Lakini Koke ni kipenzi cha klabu hiyo na Filipe Luis na rafiki wa kocha Simeone, hali ambayo inaweza kuwafanya wabaki.
Simeone amesema: "Tutakuwa na mapumziko ya kutosha, kuangalia Kombe la Dunia na kisha tutarejea kutetea ubingwa wetu wa Ligi,".