NYUMBA YA MSHIRIKI WA KILL MUSIC AWARD 2014 YAUNGUA MOTO
Nyumba ya familia ya mzee Beatus Linda iliyopo maeneo ya Igoma-Kusini mkoani Mwanza iliwaka moto na kusababisha uharibifu wa mali zilizokuwemo humo.
Moto huo uliosababishwa na gesi jioni ya saa 11 siku ya Jumanne tarehe 4-4-2014 mtaa wa Dr Sheikh Ramadhan Panzi Igoma Kusini.
Mmoja kati ya watu waliopatwa na janga hilo na mtoto wa mzee Beatus Linda ambaye ni mshiriki wa Kilimanjaro Music Award 2014 Batarokota ambaye wimbo wake wa Kwejaga Nyangisha ulishirikishwa.
Akizungumza na mwandishi wetu aliyepo Mwanza, Batarokota amesema hadi sasa familia yake inaishi nje baada ya nyumba yao kuungua na moto tangia siku hiyo na wameanza rasmi harakati za kuijenga upya.
Batarokota ameiomba serikali kuwasaidia ujenzi huo pamoja na kampuni ya bia ya Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla, 'Kusema kweli familia yangu haina uwezo wa kuijenga kwa kiwango chote nyumba hii ila nawaomba sana Watanzania wenzangu mtusaidie', alisema.
Aidha msanii huyo anayeimba nyimbo za kisukuma amewataka Watanzania wenye moyo na walioguswa na madhila ya moto wawatumie walichonacho iwe fedha, matofali, mabati kwa kuwapigia simu namba 0768-015430, au kwa njia ya M-Pesa, Tigopesa na Airtel Money.
Ambapo ametambulisha namba za kuwatumia fedha na akaunti ya benki ambazo ni M-Pesa 0763 015439, Airtel Money 0783-492623, Tigopesa 0655 492623 akaunti ya benki ya NMB ni 015201024580.